Benki ya NMB makao makuu imewezesha kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ili kujijengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mafunzo hayo ya namna bora ya utoaji huduma kwa wateja yamefanyika siku ya jumanne mwezi huu katika ofisi za NMB makao makuu zilizopo kwenye jiji la Dar es salaam na yalihudhuriwa na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kutoka Masjala,masekretari na wahudumu.
Awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mussa L. Gama ameishukuru benki ya NMB kwa kupokea na kukubali maombi yetu ya mafunzo na kuomba salamu nyingi zimfikie mkurugenzi mkuu wa NMB.
Mkurugenzi mtendaji amesema sababu zilizomfanya kuomba nafasi ya watumishi wa halmashauri kuja kupata mafunzo ya utoaji huduma katika benki ya NMB ni mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika katika taasisi hiyo na kuweza kuleta muonekano ulio bora katika utoji wa huduma kwa wananchi wote na kuifanya benki kuwa bora kabisa katika taassisi za utoaji huduma wa kifedha.
Wakati wa kuwakaribisha wageni kuhudhuria mafunzo hayo Mkuu wa Biashara za Serikali Bi Vicky Bishugu amewakaribisha watumishi hao na kuonyesha furaha kubwa waliyo nayo kwa kuona kuwa kwa sasa huduma zao wanazozitoa kwa wananchi zimekuwa bora na zinakubalika kiasi cha taasisi za serikali kwenda kupata mafunzo na uzoefu katka kutoa huduma zilizo bora.
‘Nashukuru na nimefurahi kwa kuja kwenu kupata uzoefu wa namna bora ya utoaji huduma zinzazotolewa na benki yetu.Hali hii inatudhihirishia sisi kuwa huduma zetu zipo bora na zinakubalika” Alisema Bi Vicky Bushugu.
Msafara wa watumishi waliokwenda kupata mafunzo hayo pia uliambatana na maafisa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe ambao ni Ajisa Utumishi Ndugu Patric Saduka,Afisa Tehama na Uhusiano Ndugu Mfaume Jeta na Afisa Habari wa Halmashauri Ndugu David Kambanyuma.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.