RAIS DKT SAMIA ANAWAPENDA MNO WALIMU WA KISARAWE-MHE DC NYANGASA
Kisarawe Pwani
Mkuu wa Wilaya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA Leo 21.12.2023 amekabidhi Vifaa vya TEHAMA Kwa vituo vya walimu vya Mzenga na Chanzige,
Serikali ya awamu ya sita imetoa vifaa hivi vya TEHAMA kwa lengo la Kuboresha Mazingira ya ufundishaji kwa walimu na wanafunzi hivyo natoa wito hivi Vifaa vya TEHAMA mkavitumie Kwa umakini mkubwa MNO alisisitiza MHE NYANGASA,
Aidha MHE NYANGASA alitoa hamasa kwa walimu hao kuendelea kuwatumikia watanzania kwa uadilifu Sambamba na kuwapongeza walimu hao kwa Kuongeza ufaulu kwa wanafunzi mpaka kufikia asilimia zaidi ya 85% kwa Sasa katika ufaulu,
"Binafsi nafarijika mno japo Kuna Changamoto nyingi lakini walimu mmekua vinara katika kuhakikisha mnafanya vizuri kwa wanafunzi kufaulu ili waendelee na ufaulu Mzuri" alimalizia MHE NYANGASA,
Nae akizungumza Wakati wa Hafla hiyo Mkuu wa idara ya Elimu Msingi na Awali MWALIMU HADIJA MWINUKA alisisitiza Kwa walimu hao wa vituo vya za Mzenga na Chanzige kuvitunza Vifaa hivyo TEHAMA kutoka katika GPE-LANES.II.
GPE-LANES.II. imeboresha Mazingira Bora ya kufundishia na kujifunzia katika vituo vya walimu Mzenga na Chanzige (TRC) kwa Mwaka 2023/2024 kwa kutoa Vifaa mbalimbali vya TEHAMA Kama (CPU 7, MONITORS 7, KEYBOARD 7,UPS 7, PROJECTOR 2, )
Matukio mbalimbali ya picha na Video Wakati wa Hafla ya kukabidhi Vifaa vya TEHAMA Kwa center za Mzenga na Chanzige Leo Iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.