• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Kisarawe District Council
Kisarawe District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Kisarawe District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Stategic
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Statistics
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Agriculture and Irrigation
      • Livestock and Fisheries
      • Trade and Finance
      • Works and Fire Resque
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Community Development
      • Environment and Cleanliness
      • Health
    • Units
      • Legal
      • TEHAMA NA UHUSIANO
      • Internal Audit
      • Procurement and Supplier
      • Election
      • Beekeping
    • Programu
      • TASAF
      • UKIMWI
  • Investiments
    • Tourism Attractions
      • Traditional attractions
      • Cultural Attractions
      • Natural attractions
    • Agriculture
    • Pastoralism
    • Mineral
    • Teknolojia
    • Industries
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • livestock
  • Councillors
    • Councilors List
    • Council Committee
      • Finance, Administration and Planning
      • Economic, Construction and Environment
      • Council Multisectral Aids
      • Disciplinary
      • Social Welfare
    • Meeting Timetable
    • Chairman Timetable
  • Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
    • Projects to be Implemented
  • Publications
    • By law
    • Customer Services Aggrement
    • Strategic Plan
    • Other Reports
    • Other Forms
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Photo Gallery
    • Public Notice
    • Official and National Video
    • Press Release
    • Leaders Speech

Tutimize Wajibu Wetu ‘TUSIPOE’

Posted on: June 7th, 2018

Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 ilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania mwezi april 2010 na kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 mei 2010.

Tujiulize?  Hata kwa sauti tuwaze!  Ni nani haswa anayepaswa kusimamia sheria hii? Je ni bunge ambalo ndio waliotunga sheria hii? Je ni serikali au Mahakama ambayo kisheria na kimamlaka ndio wasimamizi wakubwa wa sheria zetu tunazozitunga? au ni jamii ambayo tunaguswa na changamoto hizi au ni walemavu? NINI TUFANYE?

Kwanza sisi  tukiwa jamii inatupasa tutambue tangu awali viashiria  vya utambuzi wa watoto wenye ulemavu,Hii itasaidia kuweza  kujua mapema athari zilizopo na pengine kuweza kuepuka au kupunguza athari kwani baadhi ya matatizo ya ulemavu yanaweza kutibika  na kuepukika iwapo utambuzi utafanyika mapema  kwa watoto.

Ulemavu ni hali inayotokana na upungufu katika viungo vya mwili,vya akili na milango ya fahamu ambayo inampunguzia mtu uwezo na fursa hasa hali hiyo inapokutana na vikwazo katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika jamii.

Katika hali ya kuthaminiana,kujali utu na heshima ya mwanadamu ambapo watanzania ndiyo jadi yetu, suala linalotugusa jamii bila kujali itikadi,rangi kabila wala imani tunapaswa kuwajibika kwa pamoja na sio suala la kuwaachia taasisi,asasi, kikundi au serikali kuwajibika katika kulinda na kutetea maslahi ya kundi Fulani lenye mahitaji bali ni sote kwa pamoja.

Sheria ya watu wenye ulemavu imewekwa ikiwa na lengo la kuweka mwongozo wa kisheria wa namna ya utekelezaji utoaji huduma kwa watu wenye ulemavu,kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwa wanajamii juu ya haki za watu wenye ulemavu na kuchangamana na kushirikiana katika mazingira mbalimbali ya kazi ,kijamii na fursa za kiuchumi,

Pia kukuza uelewa miongoni mwa jamii juu ya wajibu na majukumu ya kila mwananchi na mamlaka mbalimbali za kijamii kuhakikisha haki na fursa za watu wenye ulemavu zinaimarishwa ili kujenga jamii jumuishi inayowakubali watu wa aina zote.

Mara nyingi kunapotokea tukio la kuwakutanisha pamoja watu wenye ulemavu na wale wasio walemavu ni dhahiri jamii ya wasio na ulemavu tumeshuhudia wakisononeshwa na kuhuzunishwa na hali waliyo nayo walemavu.Basi kama ndivyo, huzuni hii isiwe inaishia kwa kuwaonea huruma tu bali pia itukumbushe wajibu wetu wana jamii jukumu la kuhakikisha tunawahudumia , kushirikiana na kuchangamana nao si kwa sababu sheria imetaka iwe hivyo bali ni hiari ya lazima ya kutimiza wajibu wetu kutoka ndani ya mioyo yetu .(nafsi zetu) 

Nafsi zetu zitukumbushe kuwa tuna wajibu wa kukomesha ubaguzi na kuleta usawa,wajibu wa kutoa msaada wa kijamii kwa watu wenye ulemavu,wajibu wa kuwalinda na wajibu wa kutoa ajira na kuendeleza ajira kwa watu wenye ulemavu.

Katika kutekeleza wajibu na matakwa ya sheria hii inatupasa sote kwa pamoja tuwajibike huku tukiwa na furaha mioyoni mwetu kwa tendo la kishujaa tunalofanya kama ilivyo kwa baadhi ya taasisi.asasi na serikali inavyawajibika katika hili.

Mfano Hai,Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa Pwani imedhamiria na kuanza kutekeleza wajibu wake kwa kuwapatia watu wote wenye ulemavu Wilaya ya Kisarawe bima ya afya ambayo itawawezesha walemavu kupata matibabu bure kwenye Zahanati,Vituo vya afya na Hospitali zilizopo Wilaya ya Kisarawe.  

Kitendo hiki kitapunguza mzigo mzito waliokuwa nao walemavu katika kugharamia huduma ya matibabu kwani kama tunavyojua gharama za matibabu ni ghali sana si kwa walemavu pekee bali hata kwa watu walio na utimamu wa viungo na akili.

Kwa kuhitimisha napenda kunukuu kauli ya mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya walemavu Tanzania SHIVYAWATA bi Ummy Nderiananga kama ifuatavyo’’Niwageukie wenzangu wenye ulemavu,kwa vipawa tulivyojaaliwa na mwenyezi mungu naomba tujitaidi kuzichangamkia  fursa zilizopo katika maeneo yetu.Nawatia moyo nikiwaambia kuwa tunaweza, sisi viongozi wenu tupo pamoja nanyi’’

SISI tunawapenda,tunawajali na kuwalinda .Ndugu zangu, walemavu wasioona,viziwi,walemavu wa ngozi,walemavu wa akili,viungo, wagonjwa wa akili,walioumia uti wa mgongo na walemavu wa Mbalanga mbalanga Chepechepe tunawapenda, tuchangamkie fursa zilizopo mbele yetu kwani nguvu zenu kwa umoja wenu ni chachu kwetu jamii nzima ya Watanzania .  

By  dkambanyuma

 

 

  

Announcements

  • Wito Kwenye Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari tarehe 10-11/02/2025 Minaki Sekondari. February 07, 2025
  • Tangazo kwa Umma Kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura February 08, 2025
  • MKITANO WA BARAZA LA MADIWANI April 28, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 2021 November 09, 2021
  • View All

Latest News

  • NIMEFURAHISHWA NA MMLIVYOJIPANGA KISARAWE CHATANDA NA ZAINABU

    May 08, 2025
  • OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS SERIKALI MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA KISARAWE

    April 30, 2025
  • KISARAWE YAFANYA UTOAJI ELIMU YA DOZI YA NYONGEZA YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO(IPV2)

    April 30, 2025
  • KUVUNJWA KWA BARAZA LA MADIWANI KISARAWE UONGOZI WAJIVUNIA KUKAMILISHA MIRADI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5

    April 29, 2025
  • View All

Video

Kamati ya Fedha kutembelea Ujenzi wa Jengo Jipya la OPD Kisarawe Hospitali
More Videos

Quick Links

  • Natural Attractions
  • COMMUNITY HEALTH FUND
  • Kisarawe History
  • Photo Events in the Council
  • Rehabilitation of Theater Block
  • Council strategics
  • How to meet with District Chairman
  • Maelekezo jinsi ya kutumia Mfumo wa FFARS
  • Councilors Name List and Phone Number

Related Links

  • President's Office Public Service, Management and Good Governance
  • The National Examinations Council Of Tanzania
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • The Higher Education Students’ Loans Board
  • PPRA
  • State House
  • Employment
  • National Bureau Of statistics
  • Salary slip potral
  • Government Website
  • Parliament
  • Mfumo wa Ununuzi wa Umma NeST
  • Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (ESS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.