UBA YAIPATIA VITABU VYA KINGEREZA KISARAWE
Katika kuunga jitihada za TOKOMEZA ZERO kisarawe ili kuwa na matokeo mazuri ya masomo shuleni kwa vijana wa sekondari ambao hupatwa na changamoto mbalimbali za masomo. United Bank of Afrika [U.B.A] imetoa msaada wa vitabu vya aina tano za RIWAYA za KINGEREZA kisarawe
Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Mkurugeni Mtendaji Kisarawe Afisa Elimu Sekondari Mwalimu PATRICK MWIHAVA ameishukuru Bank hiyo ya U.B.A kwa kuisaidia KISARAWE vitabu hivyo kwa ajili ya wanafunzi ambao wanauhitaji navyo vitabu hivyo ambavyo vimetolewa bure
‘’Asanteni sana uwongozi wa Bank wa U.B.A kwa msaada huu ambao umekuja kwa wakati kwa vijana wetu hawa ambao kwa sasa wanakabiiwa na mtihani ya masomo ya mihula ambapo kupitia vitabu hivi wataenda kusoma kwa bidii ’’ alisisitiza Mwihava
Nae Afisa U.B.A FLAVIA KIYANGA alishukuru Halmashauri ya wilaya ya kisarawe kwa ushirikiano uliopo baina ya viongozi na wanafunzi mpaka kupelekea wao U.B.A kuja kusaidia kisarawe
‘’Tumevutiwa sana kuja hapa kisarawe kutokana na ushiriano uliopo baina ya viongozi na wanafunzi kwa kweli tunawapongeza na kama U.B.A tumetoa vitabu hivi kama motisha ili kuuunga mkono jitihada za viongozi na wanakisarawe za kutokomeza ZERO ’’alisema KIYANGA
Jumla ya vitabu 976 vilitolewa na UBA kwa wanafunzi wa shule za SEKONDARI YA KIMANI NA MAKURUNGE.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.