BAL0ZI wa shelisheli nchini Ms Maryvonne Pool ametoa jumla ya shilingi milioni moja na laki tano 1,500,000/ kwa ajili ya kusaidia makazi bora ya watoto Gracious Mkono na Precious Mkono waliozaliwa wakiwa wamegandana na kufanyiwa upasuaji mkubwa na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili . Akipokea msaaada huo kwa niaba ya wazazi,
MKUU waWwilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Joketi Mwegelo aliushukuru ubalozi huo kwa kazi na nia safi kabisa ya kuisaidia familia hiyo hasa kipindi hiki kigumu cha Malezi na makuzi ya watoto hao.
Aidha ubalozi huo wa shelisheli umechangia ukarabati na ujenzi wa Madarasa mawili ya kisasa katika shule ya Msingi Marui Mipera iliyopo kata ya Marui Kijiji cha Marui Mipera ambayo yalibomoka kutokana na upepo. Pia ubalozi wa Shelisheli umefanikisha uchimbaji wa kisima cha kisasa cha maji safi na salama kwa kijiji cha Kurui Kata ya Kurui katika shule ya msingi Kurui ambayo kwa muda mrefu wanafunzi wa eneo hilo wanasumbuliwa na shida ya maji safi na salama.
Balozi Ms Maryvonne ameahidi kuchangia mifuko ya saruji mia moja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya Msingi Kurui.Pia amesema ataendelea kuchangia huduma za maendeleo kadiri ya shughuli na mahitaji yanapohitajika.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.