Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA yanayoshirikisha shule za msingi ngazi ya Wilaya ya kisarawe yanatarajiwa kuanza siku ya ijumaa tarehe 01juni hadi 03 juni 2018 katika Tarafa ya Maneromango .
Mashindano hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Maneromango yatashindanisha Tarafa nne zinazounda Wilaya ya Kisarawe ambazo ni Tarafa ya Chole,Mzenga,Sungwi na Maneromango.
Michezo itakayochezwa kwenye michuano ya UMITASHUMTA mwaka huu ni riadha,mpira wa miguu,mpira wa Pete,Mpira wa mikono,mpira wa wavu pamoja na kushindanisha sanaa za maonyesho ambazo zinahusisha kwaya,ngoma ngonjera na mashairi.
Aidha baada ya mashindano hayo kumalizika itaundwa timu ya Wilaya ya kisarawe katika kila nyanja kwa kuchagua wanamichezo hodari walioshiriki mashindano hayo na watakaa kambini kujiandaa na mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa.Kambi hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 04 juni hadi 06 juni 2018 na timu itasafiri kwenda Kibaha kushiriki mashindano ya Mkoa yatakayofanyika katika shule ya Filbert Bayi.
Awali kabla ya kuanza kwa michuano hiyo kutakuwa na hafla ya kuadhimisha juma la elimu lenye lengo la kufanya tathmini ya usimamizi na utekelezaji wa ufundishaji wa stadi za kusoma ,kuhesabu na kuandika (kkk) ambapo kwa mwaka huu yataenda sambamba na michuano ya umitashumta yatakayofanyika tarafa ya maneromango na yatafunguliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya kisarawe Mheshimiwa Hamisi Dikupatile ambaye ataongozana na viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya.
By dkambanyuma.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.