1. Historia
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutekeleza mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kuanzia mwaka 2000, ikiwa ni moja ya mbinu za kutokomeza umasikini ambazo pia zilisaidia ajenda ya ugatuaji wa madaraka. Katika kipindi cha 2009 - 2012, TASAF ilifanya majaribio ya uhawilishaji fedha taslimu kwa masharti – Conditional Cash Tranfer (CCT). Majaribio hayo yalifanyika katika Wilaya za Kibaha, Bagamoyo na Chamwino za Tanzania Bara.
Tathimini ya matokeo ya majaribio hayo ilionesha mafanikio makubwa katika sekta za afya, elimu na kuongezeka kwa rasilimali za kaya. Kutokana na misingi hii afua za TASAF zilizokuwa zinatumika hapo awali zimebadilika kuwa mfumo wa kinga ya jamii tangu mwaka 2012 kwa utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - Productive Social Safety Net (PSSN I)
Madhumuni ya PSSN I yalikuwa ni kuziwezesha kaya masikini kuongeza vipato na fursa za kujikimu. PSSN I (2013 – 2019) ilifikia malengo kwa kusajili kaya 1,000,000 kutoka vijiji 10,000 kwenye Mamlaka za Utekelezaji 161 za eneo la Mradi (Jiji/Manispaa/Wilaya/Halmashauri za Miji na Unguja na Pemba kwa upande wa Zanzibar
2.HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE
Utekelezaji wa mpango ulianza mwezi Septemba 2015 ikiwa na vijiji 49 (70%) ambapo jumla ya walengwa walikuwa 2120.
Mnamo mwaka 2021 lilifanyika zoezi la uibuaji vijiji 27 (30%) vikaongezeka na kijiji kimoja kilihamishwa kutoka Manispaa ya Ubungo kuja Kisarawe na ikaleta jumla ya vijiji 28 vilivyoongezeka..
3. Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini - Kipindi Cha Pili Cha Awamu Ya Tatu
Kipindi cha Pili cha TASAF Awamu ya Tatu ni cha miaka minne kuanzia 2020 hadi 2023. Kipindi hiki kinatekelezwa katika Kata 17, katika vijiji 77 tu.
Kaya za walengwa wa Mpango katika kipindi hiki ni zaidi ya 3,000, na wanapokea ruzuku na ujira kwa njia ya tasilimu na kielektroniki.
Madhumuni ya Kipindi cha Pili ni kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa na kulinda maslahi ya watoto wao.
Kipindi cha Pili kitafikia malengo yake kwa kutekeleza shughuli mbalimbali kupitia sehemu kuu tatu ambazo ni;-
4.Sehemu za mpango
4.1 UHAWILISHAJI FEDHA (CCT)
Mpango wa uhawilishaji fedha kwa kaya maskini unalenga kutoa ruzuku kwa kaya za walengwa ili kuziwezesha kaya hizo kumudu gharama za maisha na kupata mahitaji ya msingi.
Mpango una aina kuu mbili za ruzuku ambazo ni ruzuku ya Msingi na ruzuku ya masharti. Katika Wilaya ya Kisarawe ruzuku hizi zinahaulishwa kwa njia mbili: Tasilimu na Mtandao, ambapo jumla ya kaya 865 kati ya kaya 3,005 zimejiunga na malipo kwa njia ya mtandao na kaya zilizosalia 2,140 bado zinapokea ruzuku zao kwa njia ya taslimu. Aidha elimu inaendelea kutolewa kuhakikisha kuwa kaya zote zinajiunga na njia ya mtandao.
Hadi kufikia kipindi cha malipo cha Mei – Juni 2023 jumla ya mizunguko ya malipo 39 imefanyika na kiasi cha Sh. 3,467,559,712.01 zimehaulishwa kwa walengwa wa Mpango katika wilaya ya Kisarawe.
4.2 RUZUKU YA MSINGI
Ruzuku ya Msingi ni ruzuku inayotolewa kwa kaya zote zilizotambuliwa na kuandikishwa wakati wa zoezi la uibuaji na uandikishaji wa kaya maskini. Kiwango cha ruzuku ya msingi kwa kaya ni Sh. 24,000 kwa mzunguko kwa kaya isiyo na watoto, Sh. 110,000 kwa kaya yenye watoto wa shule na walio na umri wa chini ya miaka 18.
4.3 RUZUKU YA MASHARTI
Ruzuku ya masharti ni ruzuku inayotolewa kwa kaya zenye wanakaya wenye umri chini ya miaka 5 wanaohudhuria kliniki na wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari.
5. MIRADI YA AJIRA ZA MUDA (PWP)
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe pia inatekeleza Miradi ya Kutoa Ajira ya muda kwa walengwa (PWP). Miradi hii inaziwezesha kaya za walengwa zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoibuliwa na jamii husika na kulipwa ujira. Miradi hii hutekelezwa kipindi cha hari (Septemba - Februri) pia hufanyika kwa kipindi cha miezi sita (6) ikiwa ni siku kumi (10) kwa mwezi hivyo miradi hutekelezwa kwa muda wa siku 60 kwa mwaka kwa malipo ya kiasi cha Sh 3,000 kwa siku kwa mlengwa.
Katika kipindi cha Mwaka 2022/2023 jumla ya miradi 81 ya sekta za Kilimo, Maji, Barabara, Maliasili na Mazingira ilitekelezwa yenye thamani ya Sh.419, 445,300.00 kati ya hizo Sh.340, 740,000.00 zilitengwa wa ajili ya kulipa ujira wa walengwa, Sh. 78,705,300.00 zilitumika kununulia vifaa. Mpaka kufikia malipo ya Januari-Februari 2023 kiasi cha Sh.169,512,000.00 zililipwa kwa walengwa 1,951 kwa kipindi cha Septemba, Oktoba na Novemba 2022.
Katika kipindi cha mwaka 2023/2024 jumla ya miradi 93 imeibuliwa na tayari utekelezaji wake umeanza katika vijiji vyote tangu tarehe 23/10/2023.
6. MPANGO WA KUHAMASISHA JAMII KUWEKA AKIBA NA KUKUZA UCHUMI WA KAYA. (LE)
Mpango huu unaimairisha uwezo wa kaya kufanya shughuli za kuzalisha mali hatimaye kuongeza kipato ili kujikwamua kiuchumi na kutoka kwenye umaskini kwa kuwezesha kaya kuweka Akiba na Kuwekeza.
Wilaya ya Kisarawe imewezesha kuundwa na kusajili Vikundi 98 katika Vijiji 49 kati ya 77 vyenye jumla wanachama 2248 walioweka Akiba na kukopeshana kiasi cha Sh.13, 155,500.00.
7. Habari
Taarifa Mbalimbali kwa njia ya video na Picha tembelea wenye maktaba yetu ya picha
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.