Katika Halfa hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi aliendesha zoezi la kuwaapisha Madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Kisarawe pamoja na kuendesha zoezi la uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja makamu wake.
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe asema kwamba kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma ya afya pamoja kupeleka huduma ya maji katika maeno mbali mbali hususan ya vijijini.
Hayo ameyabainisha baada ya kumalizika kwa halfa ya kuapishwa kwa madiwani wa Halmashauri hiyo ambayo ilienda sambamba na zoezi la uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti na makamu mwenyekiti ambapo amebainisha kwamba atahakikisha kwamba anashirikiana na madiwani wenzake katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Matukio kwa njia ya Picha .DSC_2953.JPG
Aidha alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba wananchi wanaondokana kabisa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta huduma ya afya pamoja na kutafuta huduma ya maji.
“Kwa kweli nashukuru Mungu nimeweza kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mwyekitiwa wa halmashauri ya Kisarawe, na mimi vipaumbele vyangu ni kuhakikisha kuwa nashirikiana na wenzangu katika kuboresha sekta huduma ya afya pamoja na masuala mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama,”alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha aliongeza kuwa nia na madhumuni yake ni kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kisarawe katika huduma mbali mbali za kijimii hivyo amewaomba madiwani wote ambao wamechaguliwa kuhakikisha kwamba wanatatua kero na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.
Naye Makamu mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mohamed Lubondo alisema kwamba atahakikisha kwamba anashirikiana kwa hali na mali na madiwani wote waliochaguliwa katika baraza jipya lengo ikiwa ni kusikiliza kero za wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuleta maendeleo chanya ya kimaendeleo.
Kwa uapande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama alisema kwamba madiwani wote ambao wameapishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria wataanza mara moja kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi katika maeneo yao mbali mbali ikiwemo kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
“Mimi kama Mkurugenzi nimeweza kuendesha zoezi la kuwasimamia madiwani 17 kutoka kata mbali mbali pamoja na madiwani wengine sita ambao ni viti maalumu, ambao wameweza kuapa kwa mujibu wa sheria na taratibu ambazo zimewekwa kwa lengo la kuweza kuanza utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi ambaye alikuwa mgeni rsami katika halfa hiyo aliwawapongeza kwa dhati madiwani wote wa Chama cha mapinduzi CCM ambao wameshinda kwa kindisndo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwataka kuwa na ushirikiano katika kutekeleza ilani ya chama kwa manufaa ya wananchi katika kuwaletea maendeleo.
“Kikubwa ambacho ninawaomba madiwani wote ambao mmeweza kuchaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni kuhakikisha kwamba mnatimiza wajibu wenu ipasavyo na kufanya kazi kwa bidii ikiwa nin utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, pamoja na viongozi wapya wa halmashauri ambao wamechaguliwa katika nafasi ya Mwemyekiti na Makamu mwenyekiti wa halmashauri,”alisema Msumi.
JUMLA ya madiwani 23 kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wameweza kuapishwa ambapo kati yao madiwani 17 kutoka katika kata zao huku wengine sita ni madiwani wa viti maalumu ambapo pia wameweza kufanya uchaguzi na kuchagua nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Makamu wake.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.