BARAZA LA MADIWANI KISARAWE LAPITISHA RASIMU YA BAJETI BIL 46 KWA MWAKA 2025/26
KISARAWE
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya bilioni 46 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Awali akisoma mapendekezo ya rasimu hiyo kwenye kikao cha baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Afisa Mipango Ndg David Moshi amesema bilioni 5.2 ya bajeti hiyo ni fedha ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
![]() |
![]() |
Aidha akizungumza mara baada ya baraza la Madiwani kujadili na kupitisha rasimu hiyo ya bajeti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mh. Zuberi Juma Kizwezwe amesema asilimia 40 ya fedha kwenye bajeti hiyo zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na asilia 60 matumizi ya kawaida kwa mapato ya ndani.
Pamoja na bajeti hii kugusa kila sekta, baadhi ya Madiwani wameeleza vipaumbele vinavyopaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee kwenye maeneo yao ambapo Diwani wa kata ya Kazimzubwi Mh. Adam Ng'imba amegusia kipaumbele cha ujenzi wa zahanati ya kifuru katika kata hiyo, huku Diwani wa kata ya Maneromango Mh. Hamis Dikupatile akizungumzia fedha za ukarabati ukumbi wa mikutano na Sherehe nyengine Katika kuboresha Mamlaka ya Mji mdogo Kisarawe.
Nae Diwani wa kata ya Marumbo Mhe Angalieni Mpendu alisisitiza kwa Baraza Hilo kuwa na Mpango wa kuendeleza Mji mdogo hasa kupima vijiji Ardhi ili kuepuka migogoro ya Ardhi pamoja na Halmashauri ya Wilaya Kisarawe kupata fedha za Ardhi iliyopimwa ,
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Petro Magoti Mh. ameendelea kusisitiza usimamizi wa Miradi ya Maendeleo huku akisikitishwa na baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika ambapo Serikali ya awamu ya sita ya Rais SAMIA imeleta fedha zote kwa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Katika miradi ya Elimu awali Msingi na Sekondari,
Kwa upande mwengine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Kisarawe KOMRED Halfani Sika alisisitiza kwa madiwani kusimamia miradi vijijini ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Katika maeneo Yao
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.