Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe yapokea msaada wa kompyuta mbili toka kwa BAYPORT FINANCIAL SERVICES.Kompyuta hizo zilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe ndugu Mussa L.Gama. Aidha Meneja wa BAYPORT kanda ya Pwani ndugu Nasri Juma na meneja wa tawi la Kisarawe walisema msaada huu umetolewa katika kutekeleza sera ya kutoa msaada kwa jamii.Mkurugenzi Mtendaji(W) alishukuru sana kwa msaada huo na kusema utasaidia sana utendaji kazi katika Halmashauri hasa katika kipindi hiki cha Teknolojia.Wadau wengine wa maendeleo wanakaribishwa kutoa misaada mbali mbali kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Zoezi hili la makabidhiano lilishuhudiwa na wakuu wa idara ndugu Anne Mwandiga ( Afisa manunuzi),Patrick Allute (Afisa Mipango) na Hafidhi Mohamed(Mtunza Hazina).
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.