Dc Jokate azindua Chanjo ya Mbwa na Paka Kitaifa Wilayani Kisarawe.Pwani
Posted on: May 5th, 2021
Dc Jokate azindua Chanjo ya Mbwa na Paka Kitaifa Wilayani Kisarawe Pwani.
Leo tarehe 05/05/2021 Mhe. Jokate Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezindua chanjo ya Mbwa na Paka Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Chanzige Kisarawe-Pwani. Wakati wa uzinduzi huo aliwashukuru wadau mbali mbali(USAID,FAO,WHO,AFROHUN,MUHAS,SUA) waliopendekeza uzinduzi huu ufanyanyike kwenye Wilaya ya Kisarawe. Pia aliwataka wananchi wote kushiriki zoezi hilo ambalo linatolewa Bure ambalo ni Takwa la kisheria kila mbwa na Paka apate chanjo hiyo.Sambamba na hilo Mgeni Rasmi Mhe. Jokate aliwakaribisha wataalam wote watakaoshiriki katika zoezi hili kutoka taasisi zote pamoja na wanachuo wa MUHAS na SUA bila kusahau aliwakaribisha wataalamu waweze kutalii katika Msitu wa Hifadhi Asilia wa kazimzumbwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kisarawe Ndugu Mussa Gama akitoa neno la shukrani kwa washiriki mbali mbali katika zoezi hili la uzinduzi wa Chanjo ya Mbwa na paka bila kuwasahau wadau toka zanzibar na kuwakaribisha tena na tena kisarawe .Ndugu Gama alisema yeye kama mwenyeji atatoa ushirikiano wote ili kuhakikisha zoezi hili linaenda kwa usalama na ufanisi ili kuleta matokeo Chanya.
Kauli Mbiu ya Zoezi hili: 'LINDA AFYA YAKO NA YA JAMII KWA KUWACHANJA MBWA NA PAKA WAKO"
Imeandaliwa na Kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO(W)-KISARAWE.