Wazazi wote Wilayani Kisarawe wafuatilie maendeleo ya watoto wao kwani ni jukumu lao,pia awataka wanapoitwa mashuleni kujua maendeleo ya watoto wao na shule kufika bila kukosa.
Aidha alimuagiza Mwenyekiti wa Halmashauri Kisarawe Mhe Hamisi Abdallah kutengeneza sheria ndogo ya faini kubwa kwa mzazi atakae kaidi wito wa shule bila ya sababu ya msingi na faini hiyo iwe chanzo cha mapato cha Halmashauri.
Maneno haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya Kisarawe Mhe:Happiness William Seneda kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya leo tarehe 31/08/2017.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.