DC NYANGASA ATOA USHAURI WA MAENDELEO YA KISARAWE KATIKA DCC
NA
KISARAWE PWANI
Mkuu wa Wilaya kisarawe Bi Fatma Nyagasa ameongoza watalaamu mbalimbali katika kikao Cha Kamati ya ushauri wa Wilaya (DCC) Leo 14.08.2023
Akizungumza wakati wa kikao kilichoendeshwa kwa Mfumo wa taalamu wa Halmashauri ya Wilaya kisarawe Kutoa ushauri Wao kwa mkuu wa Wilaya jinsi ya kuifikisha Wilaya katika Maendeleo yanayotakiwa kwa Mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM alisema Imani alonayo ni Kubwa sana kwa jamii hii ya Kisarawe kupata Maendeleo kutokana na ushauri wanaopata kutoka kwao,
"Hapa kisarawe kuna watalaamu katika fani Nyingi basi tumieni taluma zenu kuwatumikia wananchi ambao mmetumwa kwenu katika kufanya Kazi ikiwemo Elimu,Afya, umeme, Ardhi, Habari nk"
"Kupitia taluuma mbalimbali mlizonazo basi zinufaisheni Halmashauri katika kufanya Kazi kwa uzalendo na kujituma kwa weledi alisisitiza Mhe DC Nyangasa"
Hata Hivyo kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe Bi Beatrice Dominic alimhakikishia mkuu wa Wilaya kisarawe kuwa watumishi wote waliopo kisarawe wanafanya Kazi kwa umakini na Ufanisi kwa kuzingatia sheria na kanuni na Kuahidi kuleta matunda Mazuri ya Utumishi,
"Mhe Mkuu wa Wilaya kwa niaba Yao tukuhakikishie kuwa tunaenda kufanya Kazi kwa umakini na Ufanisi Mkubwa kwa maslahi ya watu wa kisarawe na taifa kwa Ujumla kama ambavyo alimalizia Bi Beatrice"
Aidha kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya kisarawe Mhe Zuberi kizwezwe, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Komred Halfani Sika, Watalaamu na Wawakilishi wa Tasisi ya Tarura,Ruwasa,Tanesco, TFS, Ardhi,TRA, Nk
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.