DED DOMINIC AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA KISARAWE
KISARAWE
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe awataka watumishi wa Halmashauri kushirikiana na kupendana katika kufanya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,
Wito huo umetolewa 20/01/2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Kisarawe Ndg. Beatrice Dominic wakati akiongea na Watumishi wa Maafisa Watendaji Kata, Vijiji ,na Wakuuu wa idara na Vitengo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Aidha Ndg Dominic ameeleza na amefafanua kwamba Watumishi wanatakiwa kufuata sharia kanuni na taratibu za kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi na kuahidi kushughulikia changamoto na kero za watumishi pindi zinapojitokeza.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji Ndg Dominic amesisitiza na kuwashauri watumishi kuachana na tabia ya majungu na kusemana na badala yake wajishughulishe na fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Hamasahuri hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi Yeniel Kagonji amewakumbusha watumishi kuzingatia sharia kanuni taratibu za kazi na kuwa na nidhamu ya kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini na kutoka kazini muda uliopangwa.
Vilevile Bw Deogratius Lokomanya ametoa rai kwa watumishi wote Halmashauri ya Kisarawe kuendelea kujifunza kwa bidii mfumo wa PEPMIS ambapo zoezi la kuingiza malengo katika mfumo bado linaendelea na kuwataka kutekeleza zoezi hilo likamilike kwa wakati sambamba na kukamilisha taratibu za Bajeti na kupanga mipango kwa wakati.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.