DKT JAFO AFUNGUA MRADI WA MAJI KITUO CHA AFYA MZENGA
Na
Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa RAIS Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amefungua Mradi wa MAJI katika Kituo Cha Afya Mzenga na kuwataka wananchi kuutunza Mradi huo,
Akiziungumza wakati wa kufungua Mradi huo wa MAJI alisema ni wajibu wa wananchi Hao wa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili uweze kudumu kwa Muda mrefu huku ukiwahudimia wananchi mbalimbali na wale wanaofika Katika kituo cha Afya Mzenga,
|
"Ndugu wananchi nimehangaika sehemu mbalimbali kutafuta wafadhili na kuwapata Hawa ndugu zetu Afrika Relief ambao wameweza kutusaidia kutatua hii kero ya maji hapa Mzenga niwashukuru sana Hawa afrika Relief kukubali kutujengea Mradi Huu mkubwa" alisisitiza Mhe Dkt Jafo
Nae Meneja wa Kanda ya Tanzania wa Taasisi ya Afrika Relief Mohamed Gewily alishukuru kisarawe kwa kupokea msaada wa Mradi huo wa MAJI alisema umegarimu Tanzania Shilingi Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini hivyo akatoa wito zaidi kwa Wanakisarawe hasa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili idumu na Kuendelea Kutoa huduma kwa Muda mrefu,
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe katika Shughuli hiyo ya Ufunguzi wa Mradi wa MAJI Ndugu Nancy Kasamala Alisisitiza kuhifadhi miundombinu ya Mradi pamoja na Kutoa wito kwa Jamii Kuendelea kutumia Kamati za maji za Vijiji katika kusimamia Mradi,
"Ndugu zangu tuliopo hapa naomba niwakumbushe jambo Moja kuna bodi ya maji Vijijini Hivyo nashauri mshirikiane na Uwongozi wa kituo Cha Afya Mzenga kwa kuendesha Mradi huu hapa ambao umejengwa hapa kituoni Kwa niaba ya Kijiji" alishauri Ndg Kasamala
Mradi Huu maji katika Tarafa ya Mzenga kata ya Mzenga Kijiji Cha Mzenga umefadhiliwa na Tasisi ya Afrika Relief wenye dhamani ya Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini unategemea kuwahudumia watu Elfu Moja mia Nne na Sitini na Tatu na pamoja watu mbalimbali wanaofika kituo Cha Afya Mzenga,
Aidha Mradi huo pia Unategemea kwa Raia kuchangia Bei ya Maji kwa Ndoo Moja ya lita Ishirini kwa Shilingi Arobaini Tu kwa Mujibu wa muongozo ili uweze kuendesha Miundombinu mbalimbali pamoja na Kukarabati.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.