DR JAFO AZINDUA MIRADI YA MAJI KISARAWE VISIMA 140 HUKU AKITAKA JAMII KUENDELEZA AJENDA YA RAIS SAMIA YA KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI
MWANDISHI WETU
Pwani-Kisarawe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amezindua mradi Mkubwa wa maji safi na Salama wa visima 140 Kisarawe 19.08.2023.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Kata ya Mzenga Mhe Dkt Jafo aliwataka Wana Kisarawe kutunza vyanzo vya maji na Mazingira ya visima ili kudumisha uhai wa visima Hivyo katika jamii,
"Natoa wito Kwa jamii ya Kisarawe na Tanzania Kwa ujumla kuyatunza Mazingira haya tusiyaharibu ili kupata maji safi na Salama Kwa muda mrefu alisisitiza Mhe Dkt Jafo"
"Lengo la visima hivi ni kuhakikisha jamii yetu haipati tabu na Inapata maji Kwa urahisi mno hivyo tuyatunze mazingira haya alimalizia Mhe Dkt Jafo"
Jumla ya visima 140 vinaendelea kuchimbwa katika Kata za Mzenga, Vihingo,Marui na Vikumburu Kwa msaada wa Taasisi na Kwa kushirikiana na Ofisi ya mbunge Jimbo la Kisarawe kwa Mwaka 2023,
Hata Hivyo akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Bi Khadija Mwinuka alishukuru Taasisi hiyo na Ofisi ya mbunge Kwa kuchimba visima vya maji karibu na Jamii na shule,
"Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe tunakupongeza sana mhe Dkt Jafo Kwa kutatulia shida hii kwa Wanafunzi wetu hasa hapa shule ya Vihingo ambapo Wanafunzi wetu wa Sekondari ya Dkt Selemani Jafo wanasoma tunaamini kabisa wataenda kufanya vyema na kuengeza wastani wa ufaulu kutokana na kupata maji alimalizia Bi Khadija
Nae kwa upande wake meneja wa mamla ya maji Kisarawe Eng Evagalista Kahwili alitoa wito Kwa jamii kutunza Mazingira pamoja na vyanzo vya maji ili jamii iwe salama na kuweza kupata maji zaidi na zaidi Kwa muda mrefu
"Ndugu zangu wa Kisarawe tunatoa wito kwenu kuungana na Mhe Rais Dkt Samia na Waziri wetu Dkt Jafo katika kusisitiza juu ya kutunza miundombinu ya visima hapa katika Kata zote za Vihingo, Mzenga, Vikumbumburu, Marui na chole ili viweze kuwahudumia Kwa muda mrefu alisisitiza Meneja Eng Kahwili"
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.