Katika kuadhimisha siku ya madaktari na Utabibu Duniani wito umetolewa kwa Madaktari wote nchini kuwa na Uzalendo wa kuwahudumia wananchi hasa wa Daraja la Chini maana Utabibu ni Wito na kazi yenye kuhitaji uzalendo na umakini wakati wote hasa kwa jamii kwarika zote za wazee,watoto na akina Mama
Akitoa wito huo kwa Madaktari leo kisarawe Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe Selemani S.Jafo amewataka chama cha madaktari bingwa nchini ‘MAT’ kuwa na moyo huo wa uzalendo kwani jamii kubwa ya watanzania wanahitaji huduma yao ya kitalaamu muda wote katika kila siku
‘’Ndugu zangu madaktari leo ni siku adhimu sana hivyo katika kuenzi siku hiii natoa ombi kwenu kuwa na moyo huo huo wa kizalendo kwa serikali yenu hasa kuwahudumia wanachi ambao wanakabiliwa na shida nyingi ambazo kuwepo kwenu hapa leo kisarawe imekua nafuu sana kwao kwani huduma mnazozitoa ni nyingi na muhimu sana mimi nikiwa kiongozi wao nasema kwa niaba yao asanteni sana mwenyenzi mungu atawalipa ’’ alisema Jafo
Aidha Jafo alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe kuhakikisha anawapatia Madaktari hao Vitendea kazi wanavyovihitaji kwa sasa, hasa wakati wa kuwapatia huduma wagonjwa wanaofika hospitalini hapo maana uwepo wa madaktari hao kisarawe ni Nadra sana hivyo ni muhimu kuwatatulia changamoto zilizopo kwa maslahi mapana ya wananchi wa kisarawe ,
‘’Mkurugenzi mtendaji wa kisarawe nimesikia changamoto za madaktari hawa nilipowatembelea wodini walikokua wanatoa huduma kwa wagonjwa waliofika naomba changamoto zao zitatue kwa wakati kwa maslahi mapana ya wanachi uwepo wa madaktari hawa wa MAT ni adimu sana kwetu kisarawe’’alisema Jafo
Naye Rais wa madaktari Tanzania Dk Elisha alisema anashukuru kwa niaba ya jopo la madaktari bingwa waliopo kisarawe na Tanzania ‘MAT’ kwa ujumla kuadhimisha siku hii muhimu kwao kwa kuongeza uzalendo wa kuwatibu watanzania wenzao hasa wenye hali ya chini kwani hujisikia fahari sana kurejesha utaalamu wao kwa watanzania wenzao ambao wanahitaji taaluma yao ya kuwatibu,
Sisi MAT tupo hapa Pwani Kisarawe kama Sehemu yetu ya Kuwahudumia Watanzania wenzetu ili kuweza kutufikia kwa urahisi ukilinganisha na unyeti wa sisi kwa pamoja timu yetu inatoa matibabu ya aina Mbalimbali ikiwemo ya Kansa ya Koo, Mkojo, Figo, Matatizo ya Uzazi kwa Mama na Baba,Sukari,Busha na Tezi Dume,
Jumla ya Wagonjwa 540 wameshahudumiwa mpaka sasa ila kila siku wananchi Zaidi wanaongezeka katika kupata huduma Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.