Hatimaye kile kilio cha muda mrefu cha wakulima wa zao la Mihogo cha kukosa mavuno stahiki kutokana na kutumia mbegu zisizo na ubora kimekwisha baada ya kupatikana kwa mbegu bora ya mhogo isiyoshambuliwa na magonjwa kwa zaidi ya asilimia 90.
MIHOGO INYOTOKANA NA MBEGU BORA YA KIBAHA 026
KIBAHA 026 mbegu ya Mhogo iliyofanyiwa utafiti wa kina na kituo cha utafiti wa mazao ya Mizizi Kibaha imethibitika kuwa ni mkombozi baada ya wakulima wa zao hilo katika wilaya ya Kisarawe kukiri kunufaika baada ya kuitumia mbegu hii.
‘kwa muda mrefu nimetumia mbegu za mihogo aina nyingi lakini nilikuwa Napata mavuno hafifu au kukosa kabisa ‘ amesema Bi Zainabu Mohamed ambaye ni mkulima wa mihogo kutoka kijiji cha Mhaga kilichopo kata ya Kibuta tarafa ya maneromango wilaya ya kisarawe.
MKULIMA WA MIHOGO BI ZAINABU AKIFAFANUA KWA KINA FAIDA ALIYOPATA BAADA YA KUTUMIA MBEGU YA MHOGO YA KIBAHA 026.
AIDHA mkulima kwa jina maarufu la Bongeambaye pia ni mkulima wa mihogo amesema ni kweli mbegu hii mpya imefanikiwa kuwahamasisha wakulima kulima kwa wingi zao hili kwani linatoa mazao mengi ambayo yanaleta faida kubwa kwa mkulima ukilinganisha na mbegu nyingine.pia ameongeza kuwa kutoshambuliwa na magonjwa ya michirizi ya kikahawia na Batobato kumewawezesha kujiamini kulima eneo kubwa zaidi kwani wana uhakika wa kuvuna alisema ndugu Bonge ambaye ana miliki shamba la mihogo lenye ukubwa wa ekari ishirini
MKULIMA WA MIHOGO NDUGU BONGE AKIELEZEA FAIDA ZA KUTUMIA MBEGU YA KIBAHA 026.
Afisa kilimo wa kata ya Kibuta ndugu Daniel Shangali akielezea kuhusu ujio wa mbegu mpya ya Kibaha one 026 amesema kipindi cha nyuma yapata miaka mitatu iliyopita zao la mihogo ilishambuliwa na ugonnjwa uliojulikana kama michirizi ya kikahawia Uliosababisha hasara kubwa kwa wananchi ingawa wenyeji walikuwa wakiuita ugonjwa wa MAKIRIKIRI kitaalamu unaitwa CASSAVA BROWN STREAK DISEASE (CBSD ) ugonjwa abao ulishambuli zao hili kwa kiasi kiasi cha kwamba wakulima walikuwa wamekata tamaa.
Aidha AFISA KILIMO aliongeza kuwa baada ya kujitokeza tatizo ili walitoa taarifa kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe na Hatimaye uongozi wa wilaya ulitafuta wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa mazao ya mizizi kutoka kibaha na ndipo walipokuja na suluhisho la kuwapatia mbegu ya KIBAHA ONE 026.
Kwa sasa serikali ya kijiji cha Mhaga kimefanikiwa kuwa na shamba la mbegu ya Mihogo ya Kibaha one 026 lenye ukubwa wa zaidi ya ekari nane inayowawezesh wakulima wa ndani na nje ya wilaya ya kisarawe kupata mbegu hiyo bora kwa urahisi.Awali wakulima wengi walikuwa wakitumia mbegu aina tofauti tofauti kama vile Rasta, Enyimba na nyinginezo zilizokuwa zinzwaletea mazao hafifu na kutishia kuacha kulima zao la mihogo kutokana na changamoto za magonywa na mavuno
AFISA KILIMO WA KATA YA KIBUTA NDU GU DANIEL SHANGALI AKIONYESHA MBEGU YA MHOGO YA KIBAHA 026
MKULIMA WA MIHOGO AKIONYESHA KIASI CHA MIHOGO INAYOPATIKANA KWENYE SHINA MOJA LA MBEGU AINA YA KIBAHA 026 NA NYUMA YAKE NI SHAMBA LAMBEGU YA MIHOGO.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.