KISARAWE IMEFIKIWA NA MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI DC NYANGASA AFURAHISHWA NA UJIO WAO GCLA.
Kisarawe Pwani.
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inaendelea na kutoa mafunzo kwa Siku tatu juu ya usimamizi na udhibiti salama wa utekelezaji wa Sheria za mamlaka maabara ya mkemia Mkuu 04/03.2024.
Akizungumza wakati wa Kufungua Mafunzo kwa wakuu wa Idara, vitengo na kamati ya Ulinzi na usalama Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA amesema utoaji wa Mafunzo na Elimu utasaidia kuwakinga wanatumishi na athari mbalimbali zinazoweza kijitokeza wakati wakifanya majukumu Yao kazini Kwa vitendo wawapo.
"Tumepata fursa ya kuwapa elimu watumishi wa Kisarawe mbalimbali kutoka Katika idara na vitengo juu ya madhara yanayopatikana na matumizi mabaya ya kemikali na jinsi ambavyo wanaweza kujikinga, pia tumetoa baadhi ya vifaa Kinga Ili watakapokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo waweze kujikinga na athari mbalimbali zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya kemikali" alisema Ndg SABANITHO MTEGA.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA amesema kuwa Mafunzo haya ya Siku mbili yatasaidia vitasaidia watumishi na wadau mbalimbali,
"Kwetu sisi Mafunzo haya ni msaada mkubwa Sana yatasaidia sana Kwa kuwa tunafahamu ofisi ya mkemia Ina Mambo mengi na Kuna kemikali ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu, hivyo watumishi wanaofundishwa watakua salama" alisema MHE FATMA NYANGASA
"Tunaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutuletea Mafunzo haya kwani ni msaada mkubwa kwetu tutaelewa juu ya elimu kemikali hatarishi tukiwa maabara" walisema watumishi watumishi
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.