KISARAWE WAFUNGUA MAFUNZO MAALUM NGAZI YA VIJIJI YANAYOLENGA NAMNA YA KUSIMAMIA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
KISARAWE.
Wasimamizi Wasaidizi wa Uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga Kura ngazi ya Vijiji Halmashauri ya Kisarawe leo tarehe *10/02/2025* wamepatiwa mafunzo maalum yanayolenga Kutoa mwongozo wa namna ya kusimamia Shughuli za Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Uchaguzi Mkuu,
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Akifungua mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Minaki iliyopo kata ya Kisarawe Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya Bi.Beatrice R Dominic amesema kwamba wamekutana hapo ili kupeana miongozo mbalimbali itakayo wawezesha kusimamia kwa uadilifu Uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga.
"Uandikishaji huu kinachotakiwa ni kusimamia vizuri taratibu zote za Uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga Kura kwa kuzingatia 4R za mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwaiyo leo tunawapitisha kwenye mada mbalimbali ili mkajue pindi mkipata matatizo muweze kukabiliana nazo Kupitia haya mafunzo, "alisema Dominic
Hata hivyo Dominic ameendelea kuwasisitiza washiriki hao kila mmoja kwa nafasi yake awajibike kwenye eneo lake ipasavyo kwa kuzingatia maelekezo na miongozo waliyopatiwa ili waweze kufanikisha zoezi hilo.
Mafunzo hayo pia yameenda sambamba na uapishwaji kwa washiriki hao ambapo wamekula kiapo Cha uaminifu na utunzaji Siri, pamoja na kiapo cha utii na uadilifu,
Zoezi hili la Uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga Kura Kisarawe kinatarajiwa kuanza Tarehe *13/02/2025 na kumalizika Tarehe 19/02/2025* Kwa kata zote 17 za Jimbo la Kisarawe
Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni *Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Maendeleo*
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.