KISARAWE WANZA KUTOA CHANJO YA RUBELA NA SURUA
KISARAWE PWANI.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA leo 16.02.2024 Kisarawe Katika hospital ya Wilaya amezindua Kampeni ya chanjo ya surua na rubella katika Halmashauri ya Kisarawe Uzinduzi huu umefanyika Katika hospital ya Wilaya,
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, MHE FATMA NYANGASA amesema kuwa waratibu waende wakahakikishe kwamba walengwa wote wakafikiwe kikamilifu kwa siku zilizopangwa.
Naye Mratibu wa Huduma za Chanjo M.KALALA amesema, Surua na Rubella ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa chanjo. Ameongeza kuwa, Magonjwa haya husababisha madhara makubwa kwa afya za Watoto walio na umri chini ya miaka mitano hata vifo.
Kampeni hii inaanza rasmi Januari 15, hadi Februari 18, 2024 na itahusisha watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi miaka mitano (5).
Aidha kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Katika Hafla Hiyo Diwani wa Kata ya Kisarawe MHE ABEL MUDO ametoa wito kwa wazazi wa kisarawe kujitokeza kupeleka watoto wao kupata Chanjo Katika vituo.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.