KISARAWE YAPITISHA BAJETI ZAIDI YA BILIONI 30 MWAKA WA FEDHA 2019/20
Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kupitia Baraza la Madiwani wamepitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 Yenye Dira ya Halmashauri kuwa yenye huduma na Mazingira Bora ya Uwekezaji ifikapo mwaka 2021 kwa Dhamira ya kutoa huduma Bora na kuweka Mazingira Ushirikishi Jamii Pamoja Utawala Bora kwa Maendeleo Endelevu
Akizungumza wakati wa kupitisha bajeti hiyo katika Baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Mussa Gama
alisema Vipaumbele vya halmashauri katika utekelezaji wa mpango wa bajeti hiyo kwa mwaka 2019/20 ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani,uzalishaji na kuwezesha wananchi kiuchumi ili kuongeza kipato kwa kutumia viwanda vidogo vidogo pamoja na ujenzi wa miundo mbinu kwa ajili ya huduma za jamii (maji,elimu na afya ).
Aidha alifafanua kua Halmashauri imeweka mkakati wa kuimarisha mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani kwa kuwa na mashine za kieletronik kwa ajili ya kukusanyia mapato kwenye vituo vyote vya kukusanyia mapato,
Mwisho alimalizia kwa kutaja miradi ya mkakati ya kisarawe kwa mwaka wa fedha 2019/20 kuwa ni ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho tarafa ya mzenga ,ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza drip(infusion unit),mradi wa ufyatuaji tofali.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.