LUSHU WA KISARAWE KINARA WA UFUGAJI NGOMBE BORA 2022 KWA MARA YA TANO MFULULIZO
NA
Wazir Wazir
Morogoro-Nanenane
wazirwazir6@gmail.com
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Tanga, Morogoro ,Pwani, na Dare es Salaam Yanayoendelea Morogoro wamemchangua mfugaji Ndugu Dotto Charles Lushu kutoka Lushu Ranch wilaya Kisarawe Tarafa ya mzenga kata ya Mafizi kijiji Cha Mafizi kuwa mfugaji Bora wa Mwaka 2022 was Kanda ya Mashariki,
Akitangazwa Mara baada ya kamati shindani ya kutafuta mfugaji Bora wa mifugo walikuta Lushu anaendelea kuwa mfugaji wa mfano Katika Kanda ya Mashariki,
"Tumefuatilia kwa karibu wafugaji wetu wa kanda nje ya maonesho na ndani ya Maonesho kwa vigezo vyetu vinaonesha Lushu anastahiki kuwa mshindi wetu Kwanza wa Kanda ya Mashariki Katika Ufungaji wa Ngombe wa Kisasa Katika Biashara Alisema Mjumbe wa Mashindano"
Kisarawe inaendelea kuwa Ni sehemu ya mfano kwa wafugaji Kanda Mashariki kwa kupanga baadhi ya Maeneo ya malisho ya mifugo aina ya Ngombe ,mbuzi, kondoo ,nk na kuwapatia wafugaji kupata nafasi ya kulisha na kufuga mifugo Yao kwa salama na amani kuondoa migogoro ya Ufugaji Kanda Mashariki,
"Sisi Kisarawe sehemu kubwa ya Maeneo ya Ufugaji tumetenga ili kuhakikisha ufugaji Unakua wenye tija na biashara kwa wafugaji wetu ili kupata faida ya ufugaji Bora na salama Kisarawe kuendana na Sera ya Ufugaji Bora inayoendana na ilani ya chama Cha Mapinduzi Ccm ya kuweka Mazingira salama kwa wafugaji nchini alifafanua Dkt Emmanuel"
Maonesho ya Nanenane Mwaka 2022 Yanayoendelea mkoani Morogoro yanatarajiwa kufungwa na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Hemed Abdullah na kwisha rasmi tarehe 10.08.2022.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.