SHULE BORA YATOA MAFUNZO YA HISABATI KISARAWE
Kisarawe Pwani.
Katika Hatua ya Kuboresha Utendaji,Ufaulu na Ufanisi wa mwanafunzi shuleni mradi wa shule Bora Umekuja na Uimarishaji wa Somo la Hisabati leo Kisarawe Minaki 26.09.2023 Mkoa wa Pwani.
Akizungumza Wakati wa kufungua mafunzo elekezi ya SoMo la Hisabati kwa Wilaya Kisarawe Afisa Mdhibiti Ubora wa Shule wa Wilaya Bi Mbwelu Emanuel Mwankina alifurahishwa na Uwepo wa Mada ya Hisabati katika Mafunzo,
"Binafsi nimefurahishwa na Uwepo wa Mada ya Somo la Hisabati katika Mafunzo haya maana imekua Changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi hasa Kisarawe" alimazia Bi Mwankina
Aidha kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi Bi Lulu Ndali alisema mafunzo hayo yakawe chachu ya mafanikio kwa Walimu kukaa pamoja kwa wingi na kubadilishana mbinu za Ufaulu na Ufundishaji wa Somo la Hisabati,
Mafunzo haya kwa Walimu kuhusu Uboreshaji wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Umahiri wenye Changamoto katika Somo la Hisabati Mkoa wa Pwani Wilaya Kisarawe kwa ufadhili wa watu wa Uingereza(UK Aid)
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.