Tarehe 05/07/2025 Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wameshiriki katika mafunzo ya Mfumo wa e- utendaji yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Mafunzo hayo yalijumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Waganga Wafawidhi, Watendaji Kata, Pamoja na Walimu wakuu. Washiriki wa mafunzo walipata fursa ya kukumbushwa(Refresher Training) moduli mbalimbali za Mfumo wa e- utendaji.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkuu wa Idara ya Utumishi na Usimamizi wa Rasilimali watu Bi. Sabra Mwankenja aliwaelekeza watumishi hao kuwa zoezi la Utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2024/2025 limeisha tarehe 30 Juni 2025 na dirisha la sasa ni Tathimini(Employee Perfomance Assessment) hivyo wahakikishe wanawafanya Tathimini kwa watumishi wanaowasimamia kabla ya tarehe 14 Julai ambapo ndo mwisho wa zoezi la Tathmini na kuwakumbusha kusimamia haki katika zoezi hilo.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.