Maktaba bora zaidi imezinduliwa na Mhe.Naibu waziri OR-TAMISEMI kwenye shule ya msingi na sekondari ya Chanzige iliyopo kata ya Kisarawe Wilaya ya Kisarawe tarehe 06/10/2017.
Maktaba ambayo ukarabati wake umechukua kiasi cha fedha shilingi milioni 34 ambazo zimetolewa na Champion Chanzige UK.Kiwango cha pesa kilichotolewa kimewezesha kugharamia uwekaji wa samani, ununuzi wa vitabu pamoja na mafunzo kwa walimu 21 juu ya matumizi ya maktaba na mbinu ya uhamasishaji wa wasomaji wa vitabu kwa wanafunzi na utunzaji wa vitabu.
Akisoma taarifa fupi ya maktaba mbele ya mhe.Naibu waziri OR-TAMISEMI Selemani Jaffo mwenyekiti wa bodi ya Champion Chanzige Organization ndugu Jackson Joseph amesema maktaba ina jumla ya vitabu vya kiada 960 kwa ajili ya sekondari,vitabu 750 kwa ajili ya shule ya msingi,vitabu vya Fiction 400,modeli tano za kufundishia masomo ya sayansi na modeli nyinginezo ambazo zinatunzwa kwenye resources cupboard.
Pia kwa mwaka 2017/2018 Taasisi ya Champion Chanzige imepanga kutekeleza miradi mingine ambayo ni kufanya ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi chanzige B,kuanzisha miradi ya kujiongezea kipato katika shule za msingi nne,kutengeneza maktaba nyingine eneo la masaki au mzenga na kufanya mradi wa uboreshaji wa kujifunza katika shule tano za kata ya masaki na msimbu kwa kushirikiana na shirika la Plan International.
Aidha mwenyekiti wa bodi amewashukuru Champion Chanzige UK wakiongozwa na madam Philippa kwa kuwezesha kufanikisha miradi yote pamoja na viongozi wa Serikali ya Wilaya kwa ngazi zote wakiongozwa na Mheshimiwa mkuu wa Wilaya Happiness Seneda kwa ushauri na kuwaongoza kufanikisha miradi hii.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.