MBIO ZA UBUNGE JIMBO LA KISARAWE ZAANZA RASMI KWA VYAMA VYA SIASA KUCHUKUA FOMU ZA INEC
KISARAWE.
Msimamizi wa uchaguzi Bi.sabra Charles Mwankenja amepokea utambulisho wa mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la kisarawe kupitia chama cha United People Democratic party( UPDP) Ndg. Athumani Ramadhani Athumani leo hii 14 agosti 2025,
Akizungumza katika ofisi ya tume ya uchaguzi Bi.Sabra Mwankenja amewaomba wagombea walioidhinishwa na vyama vyao kuchukua fomu katika ofisi ya tume ya uchaguzi katika jimbo la kisarawe kwa wakati kutoka Saa 1 asubuhi mpaka Saa 10 alasiri,
"Niwaombe watia nia wote ambao wameridhiwa na vyama vyao vya kisiasa waje kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la kisarawe katika ofisi zetu za tume"
![]() |
![]() |
Aidha Bi.Sabra Mwankenja pamoja na maafisa mbalimbali wa tume ya uchaguzi wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wagombea wote lakini pia amewataka wagombea kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu
Mgombea ubunge kupitia chama cha United people Democratic party amekuwa wa kwanza kuchukua fomu hizo baada ya dirisha la uchukuaji fomu kufunguliwa rasmi leo 14/08/2025.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.