MKURUGENZI ATEMBELEA MIRADI
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya ndg Mussa L Gama ametembelea miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya .
Katika ziara hiyo iliyofanyika siku ya jumatano tarehe 08/11/2017 Mkurugenzi mtendaji ametembelea miradi sita yenye thamani ya jumla ya shilingi 1,038,428,000/= ambapo baadhi ya miradi imekamilika na kuanza kutumika na miradi mingine ipo katika hatua mbalimbali za umaliziaji.
Akiwa katika kituo cha afya cha masaki Mkurugenzi mtendaji alikagua ujenzi wa korido unaoungnisha chumba cha upasuaji pamoja na wadi za wagonjwa .katika mradi huo kituo cha afya cha Masaki utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni sita laki nne na ishirini na nane elfu (6,428,000/=) kimefikia hatua ya kusimamisha msingi wa korido na hatua inayofuata ni kuweka nguzo na kupaua na mradi utakamilika mwisho wa mwezi huu wa kumi na moja
Katika mradi mwingine uliopo shule ya msingi ya Boga Mkurugenzi alikagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa,ofisi ya walimu pamoja na matundu kumi ya vyoo ambapo mradi umefikia hatua ya kupauliwa na baadae alitembelea miradi kama hii katika shule za msingi za Kitonga Mango na shule ya msingi ya Mitengwe ambapo miradi yote ipo katika hatua ya upauaji na kupiga bati.
Miradi hii mitatu ya shule ya Msingi Boga,Kitonga Mango na Mitengwe yenye jumla ya madarasa kumi na mbili,ofisi za walimu na matundu thelathini ya vyoo ina thamani ya fedha jumla ya shilingi milioni mia mbili na sabini na tatu elfu (273,000,000/=) Pamoja na nguvu na jitihada za wananchi.
Vile vile Mkurugezi ameweza kutembelea shule ya sekondari ya Maneromango ambapo utekelezaji wa miradi iliyopo kwa asilimia kubwa imekamilika na imeanza kutumika.Shule ya sekondari ya Maneromango imefanikiwa kujenga madarasa,Maktaba,Mabweni mawili,na vyoo ambapo vyote vimekamilika na vinatumika na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ni ya mchepuo wa kidato cha tano na sita.Mradi mwingine wa ujenzi wa bwalo la chakula unaendelea.Mradi huu una thamani ya shilingi milioni mia mbili na hamsini na tisa elfu (259,000,000)
Aidha Mkurugenzi ametembelea mradi wa ujenzi unaoendelea katika kituo cha afya cha Maneromango ambapo ujenzi uaendelea kwa kasi ya kuridhisha na ipo katika hatua ya upauaji na mradi utakapomalizika utakuwa wodi ya wazazi,Maabara,chumba cha upasuaji,nyumba ya daktari na jengo la kuhifadhia maiti ambapo thamani yak e ni jumla ya fedha shilingi milioni mia tano(500,000,000/=)
Katika ziara hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya aliongozana na Mhandisi wa ujenzi Eng. Ernest Maungo,kaimu Afisa Mipango na Takwimu ndg Ombeni Kasayo na Afisa Habari ndg David Kambanyuma pia alifanikiwa kutembelea ghala la kuhifadhia Mazao la AMCOS lililopo Maneromango ambapo shughuli za ukusanyaji wa zao la korosho na mnada unafanyika kwa sasa.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi amesisitiza kufanya kazi kwa bidii na kasi inayoridhisha na kusema kuwa miradi ya Kituo cha afya cha masaki, shule ya Msingi Boga,Kitonga Mango na Mitengwe anataka akabidhiwe ifikapo mwisho wa mwezi huu wa kumi na moja 2017 HABARI PICHA
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.