MKUU WA WILAYA YA KISARAWE AMEHITIMISHA RASMI MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA (MGAMBO)KISARAWE
Mafunzo ya jeshi la akiba yamehitimishwa rasmi Leo tarehe 7 agosti 2025 na Mhe Petro magoti mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hafla iliyofanyika katika kiwanja Cha bomani huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wazazi na wananchi waliyojitokeza kwenye hafla hiyo.
![]() |
![]() |
Akihutubia wahitimu wa mafunzo hayo, Mhe. Magoti aliwapongeza kwa uvumilivu, nidhamu na uzalendo waliouonyesha katika kipindi chote cha mafunzo, akisisitiza kuwa taifa linahitaji vijana wenye moyo wa kujitolea kulinda amani na usalama wa jamii zao.
Aidha wa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo, alieleza kuwa jumla yavijana154,wamehitimumafunzo hayo ya muda wa miezi mitatu ambapo walifundishwa masuala ya ukakamavu, sheria ndogo za mtaa, mbinu za ulinzi, pamoja na maadili ya utumishi wa kujitolea.
![]() |
![]() |
Wahitimu wamefanya maonesho mafupi ya kuonesha ukakamavu wao mbele ya mgeni rasmi, huku akiwasihi kuzidi kutumikia kiapo Chao pamoja na kudumisha amani na mshikamano katika jamii.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.