Mwenge Wa UHURU 2018 Wakamilisha Ziara Yake Kisarawe Kwa Kishindo
Hatimaye Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 umekamilisha ziara katika Wilaya ya Kisarawe kwa kishindo baada ya kutembelea na kuzindua miradi iliyokidhi vigezo kwa mafanikio.
Katika ziara hiyo iliyoanzia uwaja wa ndege wa Mwalimu Julius kambarage Nyerere ulipowasili kutoka Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani mwenge ulipokelewa na Mheshimiwa Happiness Seneda mkuu wa Wilaya ya kisarawe aliyeambatana na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Kisarawe,watumishi wa Halmashuri ya Wilaya na wananchi waliojitokeza
Baada ya kupokelewa mwenge ulianza ziara yake Wilaya ya kisarawe kwa kutembelea chuo cha maendeleo ya wananchi kilichopo eneo la Sanze ambapo walishuhudia shughuli mbambali zinazofanyika hapo ikiwemo utekelezaji wa utoaji mafunzo ya ufundi stadi kwa kozi za ushonaji,ufundi Uashi,Upishi,Umakanika,Uchomeleaji na umeme wa magari na majumbani.
Baada ya hapo mwenge ulielekea shule ya Sekondari ya Seminari iliyopo kitongoji cha Sanze na kushuhudia namna ya uwekezaji katika elimu na baadaye msafara wa mwenge ukaelekea eneo la Yombo Lukinga ambapo mwenge ulizindua mradi wa madarasa, kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kutoa gawio la michango ya mwenge kwenye shughuli za maendeleo.
Aidha mwenge ulifanikiwa kutembelea kijiji cha Titu na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 421,558,894/= ambalo ni kiunganishi kati ya Kijiji cha Titu na Kijiji cha Kihare na mwenge wa Uhuru ukatembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Chole kinachogharimu kiasi cha shilingi milioni mia nne (400) ambapo mwenge ulipokea taarifa za shughuli za mapambano dhidi ya Malaria,ukimwi na madawa ya kulevya.
Vilvile mwenge wa Uhuru uliekea shule ya Sekondari ya Maneromango inayopokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kutembelea klabu ya kupambana na rushwa na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani na kisha ukaelekea ofisi ya Kata ya Maneromango na kuzindua ofisi ya kata hiyo iliyogharimu kiasi cha shilingi 26,000,000/= ambapo kati ya hizo shilingi milioni 12,460,000/= ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi 8,696,000/= fedha za ruzuku ya maendeleo kutoka Serikali kuu na kiasi cha shilingi 4,844,000/= ni nguvu za wananchi wa Maneromango.
Baada ya kukamilisha ziara hiyo mwenge wa uhuru ulielekea eneo la mkesha katika Shule ya Msingi Mitengwe Kata ya Mzenga iliyopo Tarafa ya Mzenga ambapo ilikagua mabanda ya wajasiriamali,upimaji wa virus vya ukimwi (VVU) na uthibiti wa madawa ya kulevya na pia kusoma na kusikilia risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
Katika ziara yote ya mwenge wa uhuru mwaka 2018 wananchi walijitokea maeneo yote na kushudia miradi iliyotekelezwa kwa kufuta miongozo,weledi na viwango vya hali ya juu na kuacha kumbukumbu nzuri ya kufanikisha shughuli zote kwa ufanisi.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.