NINACHOKITAKA KWENU WATAALAAMU WA HALMASHAURI SIMAMIENI MIRADI IMALIZIKE KWA WAKATI-DKT JAFO
Kisarawe Pwani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mb MHE DKT SELEMANI SAIDI JAFO Leo ameambatana na wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya katika kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo Kisarawe ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025,
Akizungumza 24.10.2023 wakati wa kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa shule mpya ya kisasa Kata ya msimbu Kijiji Cha Kitanga MHE DKT SELEMANI SAIDI JAFO alisisema,
"Lengo la ziara Yetu kwa wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya Kisarawe ni kukagua Miradi ya maendeleo kuona inasimamiwa na Kumalizika kwa Wakati Kama ilivyokusudiwa na kupatiwa Fedha na Rais DKT SAMIA Kisarawe inamaliza kwa kiwango na hatua iliyokusudiwa" alisisitiza Mhe Dkt Jafo
|
|
|
|
"Nashukuru Sana Serikali Yetu ya awamu ya sita imekua inaendelea kuipatia Kisarawe Miradi mingi mipya katika Kama Miradi ya Elimu,Afya, Maji, Miundombinu ya Barabara na Umeme basi watalamu kasimamieni na kuhakikisha imalizika kwa Wakati na kuweza kuwahudumia wananchi kwa Wakati alisisitiza Mhe Dkt Jafo
Aidha Mkuu wa Wilaya Kisarawe Mhe FATMA NYANGASA alisisitiza Suala la Jamii hasa Kisarawe kuendelea kuchukua Kwa umakini tahadhari ya kujikinga na Madhara hasa Kauli ya mamlaka ya Hali ya hewa juu ya Suala la uwepo wa Mvua Kubwa ya ELL-NINO na kuchukua hatua kwa kuhama mabondeni,
"Ndugu zangu haya maendeleo Yetu yote yanayoletwa hapa Kisarawe muhimu tuwe watu wenye kujali na kufuatilia taarifa za Serikali juu ya kuchukua tahadhari ya majanga na mapema" alisisitiza MHE NYANGASA
Aidha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Kisarawe KOMRED KHALIFAN SIKA alisisitiza kwa Mafundi,watalamu wasimamie Miradi imalizike kwa Wakati maana Kila kitu kipo basi wao watimize wajibu wao wa kuwahudumia wananchi,
"Hii Miradi Kama sisi Serikali hatudaiwi chochote na nyie ikiwemo Labda Fedha nk Wakati mwengine Fedha zote zimetoka kwa Nini nyie mnakua wazito katika kusimamia haya maendeleo Sasa Kwa kuwa sisi tupo hapa kusimamia ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM tunawaagiza wale wote wenye Miradi basi ikamalizike kwa Wakati" alisisitiza KOMRED KHALIFAN SIKA
Nae Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe NDG BEATRICE DOMINIC alishukuru Kamati ya siasa ya Wilaya Kisarawe kwa kukagua Miradi na kuahidi kutekeleza Kwa Wakati maagizo yote yaliotolewa na wajumbe Wakati wa Ukaguzi wa Miradi Kitanga,Kazimzubwi, Kisarawe na Bomani,
Jumla ya Miradi mitano imetembelewa na kukaguliwa na wajumbe wa Kamati ya siasa ya Wilaya Kisarawe Katika Kitongoji Cha Kitanga Mradi wa Shule mpya ya Sekondari, Mradi wa Bweni shule ya Sekondari Kisarawe Kitongoji Cha Kazimzubwi, Mradi wa ukarabati wa Soko la Kisarawe, Pamoja na Jengo Jipya la kisasa la utawala katika Eneo la Bomani
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.