RC KUNENGE AKUTANA NA KAMATI YA WATALAAM (CMT) HALMASHAURI YA MKURANGA NA KISARAWE KUJADILI BAJETI AWATAKA KUWA WABUNIFU KATIKA KUKUSANYA MAPATO
MKURANGA PWANI.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Alhaji Abubakar Kunenge 14.02.2024 amekutana na Kamati za Watalaam wa Halmashauri ya Mkuranga na Kisarawe katika Ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mkuranga,
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Ndg RASHIDI MSHATA alimkaribisha kuzungumza na Wataalamu hao na kuwapo tayari kupokea maelekezo yake Mkuu wa mkoa Katika kujenga TAIFA,
Mhe. Kunenge alisema kuwa lengo la Kikao kazi hicho ni kupitia na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa tarehe 31 Januari 2024,
*"Napenda niwataarifu kuwa tulipokea barua Toka Kwa Mhe. Waziri Mchengerwa yenye maelezo ya uboresha katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuongeza vyanzo vya mapato, kudhibiti upotevu wa mapato pamoja na matumizi ya fedha za maendeleo pamoja na Kuangalia maoteo na vipaumbele vya bajeti zetu 2024/2025*" Alisema Mhe. Kunenge.
Fanyeni mikakati ya Ukusanyaji mapato kuweni wabuni ukusanyaji wa tabia za Kitamaduni zimepitwa na Wakati Muhimu kuwa na Data za walipa kodi tusingananie Service levy bunini vyanzo vipya vya Mapato Katika Mazingira yetu kuweni fair msifanye hovyo watembeleeni walipa kodi wenu wapeni hata barua za apriciation kwa wateja wenu,
Nashauri kuweni wabuni Zaidi na mwisho kuweni usasa Katika kulipa kodi, alisisitiza MHE ALHAJ KUNENGE
Hii ni ziara ya kupitia bajeti za Halmashauri zote tisa za mkoa wa PWANI ambayo Mkuu wa mkoa wa PWANI MHE ALHAJ KUNENGE anazisimamia.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.