WAHESHIMIWA MADIWANI KISARAWE WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WASISITIZA KUMALIZIKA KWA WAKATI
KISARAWE.
Waheshimiwa madiwani wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kupitia kamati ya Uchumi Fedha Uongozi na Mipango wilayani Kisarawe 28/01/2025 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Zuberi Kizwezwe.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda Cha Korosho kilichopo kata ya Mzenga,Shule mpya ya Sekondari kata ya BOGA,shule ya Sekondari iliyopo Visiga,shule mpya ya Sekondari ya Gongoni pamoja na Jengo Jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Kisarawe,
Waheshimiwa Madiwani kupitia kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za kuanzisha na kuendeleza miradi hiyo katika wilaya ya Kisarawe,
Sambamba na hilo, Waheshimiwa Madiwani wamemsisitiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bi.BEATRICE DOMINIC kusimamia vizuri wa fedha za miradi ya maendeleo.
Vilevile Waheshimiwa Madiwani wamewapongeza wananchi wa kata za Boga, Mzenga na msanga kwa ushiriki Katika kufuatilia miradi iliyopo Katika kata zao pamoja na vijiji kwa kupata uelewa juu ya miradi,
Pamoja na hayo Waheshimiwa Madiwani wamemepongeza mafundi wanaosimamia miradi Hiyo kwa kuwataka kuendeleza umakini wa usimamizi wa miradi haya ya Ujenzi wa miundombinu ya shule pamoja na Vifaa kwa viwango ikiwamo Milango,madawati,viti nk.
Aidha Waheshimiwa madiwani kupitia kamati ya Fedha, wametoa maagizo kuhakikisha mradi wa Ujenzi wa kiwanda Cha Korosho Cha Mzenga kukamilika kwa wakati na kusimamiwa Kila hatua ya Ujenzi wake Kupitia ofisi ya msimamzi wa Ujenzi wa kiwanda Hicho,
Mwisho waheshimiwa madiwani wameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Kisarawe
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.