WALIMU WASHEHEREKEA MAFANIKIO
WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE WAMEFANYA SHEREHE KUBWA YA KUJIPONGEZA KWA AJILI YA MAFANIKIO WALIYOYAPATA MWAKA ULIOPITA.
SHEREHE HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA SHULE YA SEKONDARI MINAKI ILIHUDHURIWA NA WAZIRI WA OFISI YA RAIS TAWALALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MHESHIMIWA SELEMANI JAFO AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO LA KISARAWE PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WA HALMASHAURI AKIWEMO MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MHE. HAMISI DIKUPATILE, BAADHI YA WAHESHIMIWA MADIWANI NA MAAFISA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE
SHAMRASHAMRA HIZO ZIMEAMBATANA NA ZOEZI LA KUWAAGA RASMI WALIMU WASTAAFU AMBAO WAMEMALIZA MUDA WAO WA UTUMISHI ULIOTUKUKA KATIKA KUIHUDUMIA JAMII YA WANAKISARAWE. WALIMU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE WAMEWAZAWADIA ZAWADI MBALIMBALI WATUMISHI WENZAO WASTAAFU KWA KUWAPATIA ZAWADI ZA SAMANI,VYOMBO NA NYINGINEZO KWA KILA MSTAAFU.
AIDHA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI NA ZILIZOONYESHA JITIHADA ZIMEPEWA ZAWADI NA MGENI RASMI AMBAPO WALIMU VIONGOZI WA SHULE HIZO WALIPOKEA ZAWADI HIZO KWA NIABA YA WATUMISHI WENGINE WA SHULE HIZO.
AKIZUNGUMZA WAKATI WA SHEREHE MGENI RASMI AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO LA KISARAWE MHESHIMIWA SELEMANI JAFO AMEWAPONGEZA WALIMU KWA JUHUDI WANAZOFANYA KUBORESHA ELIMU NA KUAHIDI KUWA NAO SAMBAMBA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI.
AIDHA MBUNGE HUYO AMEELEZA JUHUDI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWA KUZITENGEA FEDHA BAADHI YA SHULE KUFANYA UKARABATI MKUBWA.BAADHI YA SHULE ZILIZOTENGEWA FEDHA NA KUKARABATIWA NI PAMOJA NA SHULE YA MSINGI BOGA,MITENGWE,KITONGA MANGO,KWALA NA SHULE YA SEKONDARI YA MANEROMANGO . PIA FEDHA NYINGINE ZIMETENGWA KWA SHULE NYINGINEZI IKIWEMO SHULE YA SEKONDARI KIMANI AMBAYO INATARAJIWA KUANZA KUWAPOKEA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA TANO IFIKAPO MWEZI JULAI 2018
SHEREHE HIZO ZIMEFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 24/02/2018 NA KUHUDHURIWA NA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOMO WILAYA YA KISARAWE PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA HALMASHURI YA WILAYA YA KISARAWE.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.