Watu Wenye Ulemavu Kukatiwa Bima Ya Afya Kisarawe
Katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015, sheria Na. 9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu na miongozoz mbalimbali ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapatiwa haki katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya,Utamadunu,Sanaa na Michezo watu wenye ulemavu Wilaya ya Kisarawe wanatarajia kukatiwa bima ya afya ili kuwapunguzia mzigo mkubwa wa gharama za matibabu.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mheshimiwa SELEMANI Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe wakati akikabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye Ulemavu tukio lililofanyika kwenye viwanja vya stendi kuu ya Wilaya ya Kisarawe.
Mhe. Jafo amesema jamii inapaswa kuwasaidia na kuwawezesha watu wenye ulemavu ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kwa kuzingatia hali waliyonayo ambayo inahuzunisha kuona wanapata tabu katika kuendesha maisha yao kulingana na hali zao.
‘’ Wote tumeshuhudia namna ya wenzetu hawa wanavyopata tabu kukabiliana na changamoto hizi,Mkurugenzi nakuagiza walemavu wote wa Wilaya ya kisarawe ambao idadi yao ni 1608 wakatiwe bima ya afya ambayo itawawezesha kupata huduma ya afya katika Wilaya yote ya kisarawe, na zoezi hili liwe limekamilika kufikia mwishoni mwa mwezi wa sita ‘’ alisema Mhe. Jafo huku akionyesha kuhudhunishwa na hali ya walemavu hao wakati wanashuka kwenye magari wakitokea sehemu mbalimbali za wilaya.
Wilaya ya kisarawe ina jumla ya walemavu albino 59,wenye ulemavu wa viungo 605,viziwi 347,wenye ulemavu wa akili 96,wenye ulemavu mchanganyiko 183 na wasioona 205.
Katika tukio hilo ambalo pia lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ,Mbunge wa viti maalum Mkoa wa pwani Mhe. Zainab Vulu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mhe. Hamisi Dikupatile , Madiwani na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.