ZIARA YA KATIBU WA TAGCO YALETA MATUMAINI KWA MAAFISA HABARI NJAIDI
Na Mwandishi Wetu
Katika kuhakikisha Kuwa ufanisi unapatikana katika maeneo ya kazi na Maendeleo Kwa mafisa habari na mawasiliano Serikalini Suala la Kutembeleana na Kubadilisha uzoefu ni muhimu mno hayo yamesemwa na Katibu wa TAGCO 08.10.2022,
Akiongea wakati kutembelea mabanda ya Halmashauri za Mafia, Rifiji, Kibiti, Mkuranga, Kisarawe,Kibaha Dc,Chalinze,Kibaha TC, na Bagamoyo mkoani Pwani Katibu wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Ndugu Abdul Njaidi alishauri Kwa Maafisa hao kuhakikisha Kuwa wanajituma na kufanya Kazi Kwa Weledi ili kuzitangaza na kuzitambulisha fursa zilizopo katika maeneo Yao ya kazi Kwa jamii Ili kuleta tija Kwa maendeleo ya Jamii,
"Ifikie Hatua mafisa habari na mawasiliano Serikalini mjitume Kwa Hali na Mali kuhakikisha fursa za maeneo Yenu ya kazi zinatambulika Japo Kuna ugumu fulani Hivi ambao sio Rasmi ila nyie mnapaswa kufanya Kazi Kwa vigezo na viwango alisisitiza Njaidi"
"Sisi Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika taasisi ni viungo muhimu hivyo mjitambue na mfanye kazi Ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa sawa na msiwe Watu wa kulalamika lalamika Kwa kukosa vitendea kazi kama Pc,Simu, na Camera Wewe Fanya kazi ikionekana Nzuri na imesaidia taasisi yako kiongozi wako atakupatia alifafanua Njaidi"
Hata hivyo Kwa niaba ya mafisa habari na mawasiliano Serikalini wenzake Mkoa wa Pwani Akiongea afisa habari Kisarawe Alimshukuru katibu huyo wa TAGCO kuwatembelea Kwa Umoja wao katika Mkoa wa Pwani na kumtaka afike Zaidi katika maeneo ya kazi Ili Kuona Uhalisia wa mazingira ya kazi,
*Kwa niaba ya wenzangu Pwani tumefurahishwa na ujio wako Hapa Kibaha na pia tunakuomba ufike Site Kuona Zaidi mazingira ya kazi Ili kama taasisi siku tukikaa Kuzungumza Mafanikio na changamoto zetu unazifahamu katika Kazi Pamoja na Kuona Zaidi fursa za kutangaza Zaidi Alimalizia Wazir"
Katika kuhakikisha Maonesho yanafana Kwa jamii wandishi wa habari na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wanashiriki Kwa kusaidia kuhabarisha na kutangaza fursa Kwa wanaofika katika maeneo ya Maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani kauli mbiu ya Mwaka Huu 2022 ni,
PWANI NI SEHEMU SAHIHI KWA UWEKEZAJI, PAMOJA TUJENGE VIWANDA NA AJIRA
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.