• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Kisarawe District Council
Kisarawe District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Kisarawe District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Stategic
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Statistics
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Agriculture and Irrigation
      • Livestock and Fisheries
      • Trade and Finance
      • Works and Fire Resque
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Community Development
      • Environment and Cleanliness
      • Health
    • Units
      • Legal
      • TEHAMA NA UHUSIANO
      • Internal Audit
      • Procurement and Supplier
      • Election
      • Beekeping
    • Programu
      • TASAF
      • UKIMWI
  • Investiments
    • Tourism Attractions
      • Traditional attractions
      • Cultural Attractions
      • Natural attractions
    • Agriculture
    • Pastoralism
    • Mineral
    • Teknolojia
    • Industries
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • livestock
  • Councillors
    • Councilors List
    • Council Committee
      • Finance, Administration and Planning
      • Economic, Construction and Environment
      • Council Multisectral Aids
      • Disciplinary
      • Social Welfare
    • Meeting Timetable
    • Chairman Timetable
  • Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
    • Projects to be Implemented
  • Publications
    • By law
    • Customer Services Aggrement
    • Strategic Plan
    • Other Reports
    • Other Forms
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Photo Gallery
    • Public Notice
    • Official and National Video
    • Press Release
    • Leaders Speech

Ziara Ya Mbunge Yaleta Matumaini Kwa Wananchi Kisarawe.

Posted on: September 25th, 2018

Ziara ya takribani siku tano aliyofanya Waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo La kisarawe Imeleta Hamasa kubwa na matumaini kwa wananchi wa  Kisarawe ambapo mwanga mpya wa matumaini umejitokeza kwa wananchi hao.

Katika ziara hiyo iliyofanywa kwenye Kata za Marui,Msanga,Mafizi  Vihingo na Kibuta  ilihusisha vijiji  kumi na mbili ambapo Mheshimiwa Waziri alifanya mikuatano kwa kukutana na wananchi wa vijiji hivyo kwa kuwaeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ,Mafanikio na changamoto zilizopo pamoja na kusikiliza kero,maoni na ushauri kutoka kwa wananchi hao. 

Mheshimiwa selemani Jafo amewaeleza wananchi juu ya adhma ya Serikali kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo ili wananchi wanufaike kutokana na kodi zinazokusanywa  na serikali kwa kujenga miundo mbinu na kuwaletea wananchi huduma mbalimbali.

“ Wananchi wa Kisarawe mmenipa dhamana ya kuwatumikia lakini Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania John Pombe Magufuli ameniona na kunipa dhamana kubwa ya kuwatumikia wananchi wa Nchi nzima na mimi ninawambia sitawaangusha.Tumeamua kutekeleza ilani ya Chama chetu Cha Mapinduzi kwa vitendo na sisi tuliopewa dhamana tumeamua kutekeleza kwelikweli,kwenye sekta ya Afya tumejenga miundo mbinu ya kuwezesha tunapeleka huduma za afya karibu na wananchi.tumejenga vituo vya Afya,Zahanati na tumepeleka magari ya wagonjwa sehemu mbalimbli za Wilaya yetu kwani kila kituo cha Afya kina gari ya kubebebea wagonjwa” amesema Mheshimiwa Jafo.

Aidha Mbunge wa Kiasarawe ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI amewaambia wananchi kuwa juhudi zinaendelea kufanywa katika sekta nyingi kama vile Elimu kwa Wilaya ya Kisarawe Miradi mingi imefanyika kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kujenga madarasa ,Nyumba za Walimu na vyoo ambapo Shule za Mitengwe,Boga, Kitonga Mango,Chang’ombe, Gwata Kwala na Yombo Lukinga zimejengwa Madarasa ya Kisasa pamoja na Ofisi za Walimu.

Pia katika ziara hiyo Mheshimiwa mbunge amewaambia wananchi kuwa jitihada kubwa zinafanywa na zinzendelea kufanywa katika sekta ya miundombinu ya Barabara ambapo barabara nyingi zimejengwa na kukarabatiwa  ambapo Kwa Kisarawe mjini Barabara za lami zimejengwa kwenye mitaa na barabara zinazounganisha kata na vijiji zimekarabatiwa.

“ Katika ujenzi wa barabara ya kutoka Kisarawe hadi Maneromango ambayo ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi tumeanza kuijenga kwa kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tumemaliza kilomita sita za awali na sasa tunaendelea na ujenzi wa kilomita nne na hivi karibuni tumepata kiasi cha shilingi bilioni mbili amabazo tunaziingiza kwenye ujenzi wa barabara hiyo lengo kubwa tuweze kukamilisha ujenzi wa barabara ya lami kufika Maneromango inakamilika “ Aliongeza Waziri wa TAMISEMI.

Ziara ya Mbunge wa kisarawe iliweza kumfikisha katika vijiji vya Marui Ngwata na Marui Mipera katika Kata ya Marui ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa barabara kutoka kijiji cha Msanga hadi Marui barabara ambayo imekamilika pamoja na kukgua zahanati ya Marui Ngwata ambayo inatoa huduma kwa sasa.Pia alitembelea vijiji vya Ving’andi,Gwata na Mafizi katika kata ya Mafizi na vijiji vya Chamalale,Sangwe na Kibwemwenda katika Kata ya Vihingo na kuhitimisha ziara yake kwa kuzuru vijiji vya Mtamba, Masanganya na Bwama katika kata ya Kibuta.

Ziara hiyo iliyochukua takribani siku tano kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 21 mwezi wa tisa iliambatana na Msafara wa Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia na Afisa Mipango na Takwimu Ndugu Patric Allutte pamoja na Wakuu wa idara  za Elimu Msingi Ndugu Esther Senkoro,Elimu sekondari NDUGU Kangisi,Afisa Mifugo,Afisa Kilimo,Afisa Maendeleo ya Jamii,Mhandisi wa Ujenzi,Afisa Ardhi,Mganga Mkuu wa Wilaya, Afisa Habari Ndugu David Kambanyuma,Mhandisi wa TARURA  Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kisarawe na Wataalamu kutoka Ofisi ya TARURA Makao Makuu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Barabara mijini na vijijini.

Mbunge wa Kisarawe pia aliambatana na ujumbe kamili wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Wilaya Ndugu Halfani SIka,katibu wa Chama Wilaya.Katibu Mwenezi, Mwenyekiti wa umoja wa Vijana.Mwenyekiti wa Jumuija ya Wazazi, Mhamasishaji wa vijana pamoja na Katibu wa Mbunge .

  

Announcements

  • Wito Kwenye Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari tarehe 10-11/02/2025 Minaki Sekondari. February 07, 2025
  • Tangazo kwa Umma Kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura February 08, 2025
  • MKITANO WA BARAZA LA MADIWANI April 28, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 2021 November 09, 2021
  • View All

Latest News

  • NIMEFURAHISHWA NA MMLIVYOJIPANGA KISARAWE CHATANDA NA ZAINABU

    May 08, 2025
  • OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS SERIKALI MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA KISARAWE

    April 30, 2025
  • KISARAWE YAFANYA UTOAJI ELIMU YA DOZI YA NYONGEZA YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO(IPV2)

    April 30, 2025
  • KUVUNJWA KWA BARAZA LA MADIWANI KISARAWE UONGOZI WAJIVUNIA KUKAMILISHA MIRADI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5

    April 29, 2025
  • View All

Video

Kamati ya Fedha kutembelea Ujenzi wa Jengo Jipya la OPD Kisarawe Hospitali
More Videos

Quick Links

  • Natural Attractions
  • COMMUNITY HEALTH FUND
  • Kisarawe History
  • Photo Events in the Council
  • Rehabilitation of Theater Block
  • Council strategics
  • How to meet with District Chairman
  • Maelekezo jinsi ya kutumia Mfumo wa FFARS
  • Councilors Name List and Phone Number

Related Links

  • President's Office Public Service, Management and Good Governance
  • The National Examinations Council Of Tanzania
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • The Higher Education Students’ Loans Board
  • PPRA
  • State House
  • Employment
  • National Bureau Of statistics
  • Salary slip potral
  • Government Website
  • Parliament
  • Mfumo wa Ununuzi wa Umma NeST
  • Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (ESS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.