• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Kisarawe District Council
Kisarawe District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Kisarawe District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Stategic
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Statistics
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Agriculture and Irrigation
      • Livestock and Fisheries
      • Trade and Finance
      • Works and Fire Resque
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Community Development
      • Environment and Cleanliness
      • Health
    • Units
      • Legal
      • TEHAMA NA UHUSIANO
      • Internal Audit
      • Procurement and Supplier
      • Election
      • Beekeping
    • Programu
      • TASAF
      • UKIMWI
  • Investiments
    • Tourism Attractions
      • Traditional attractions
      • Cultural Attractions
      • Natural attractions
    • Agriculture
    • Pastoralism
    • Mineral
    • Teknolojia
    • Industries
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • livestock
  • Councillors
    • Councilors List
    • Council Committee
      • Finance, Administration and Planning
      • Economic, Construction and Environment
      • Council Multisectral Aids
      • Disciplinary
      • Social Welfare
    • Meeting Timetable
    • Chairman Timetable
  • Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
    • Projects to be Implemented
  • Publications
    • By law
    • Customer Services Aggrement
    • Strategic Plan
    • Other Reports
    • Other Forms
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Photo Gallery
    • Public Notice
    • Official and National Video
    • Press Release
    • Leaders Speech

ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE KATIKA ZOEZI LA UGAWAJI WA HATI ZA KIMILA KWA WAFUGAJI.

Posted on: June 25th, 2021


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Nickson Simon John tarehe 25.06.2021 amefanya ziara ya kutembelea wafugaji na kuwakabidhi hati za kimila. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Mwanana Msumi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mhe. Zuberi Kizwezwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mussa L. Gama, Diwani wa kata ya Mafizi Mhe. Yadhamen Jafari Nghonde, Mwakilishi wa Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Pwani Ndg. Fredrck Mrema, Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mabula K. Isambula, watendaji wa kijiji na mtendaji wa Kata,pamoja na timu ya watalaam wa Ardhi na Ufugaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.


Aidha katika zoezi la ugawaji wa Hati za Kimila kwa wafugaji mwakilishi wa kamishna msaidizi wa ardhi wa mkoa wa Pwani Ndg. Fredrick Mrema alisema Hati ni ukombozi na kusisitiza kuwa  hati ni Mali.


Katibu wa wafugaji wilaya ya Kisarawe Ndg. Filipo Umundi alimshukuru Mgeni Rasmi (Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe) kwa hatua kubwa ya ugawaji wa Hati za kimila kwa wafugaji  na kumuomba kuwa zoezi hilo la ugawaji wa Hati  lifanyike kote kwani ni chachu kwa maendeleo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mussa L. Gama alimkaribisha mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Nickson Simon John, na aliwapongeza wanakijiji cha mafizi kwa kupatiwa Hati. Ndg. Gama Alisisitiza kuwa waliopewa Hati wazingatie masharti ya Hati hiyo na kudhibiti uzururaji ovyo wa wanyama, pia alimtambulisha mfugaji bora ambaye anaiwakilisha vema kisarawe, Ndg. Gama aliendelea kwa kuainisha vema kwa mkuu wa Wilaya changamoto ya mpaka kati ya wilaya Kisarawe na Wilaya ya Kibaha, na kuelezea maadhimio yaliyofikiwa kuwa mipaka imerekebishwa, kilichobakia ni kutangazwa rasmi. Amewatoa hofu wanakisarawe.


Aidha Mkuu wa Wilaya aliwapongeza wana Mafizi na wafugaji waliopatiwa Hati 24 za kimila na pia kuwakumbusha kuwa Ardhi ndo hifadhi ya maisha na alisisitiza kuwa hifadhi bora ni ile ambayo imelindwa, kisheria na kufuata taratibu na kanuni, Mhe. Nickson alisema kuwa kama wafugaji wana hati na wamesajiliwa inajenga msingi mzuri kwa wafugaji, mana serikali itajua idadi ya mifugo na ukubwa wa ardhi waliopewa. Pia alisema kuwa mali yenye thamani ni ile mali inayotambulika, inaweza kulindwa na kuendelezwa.


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alisititiza kuwa kila haki inaambatana na wajibu, amewaasa wafugaji kuheshishimu mipaka, amewaomba wafugaji kuelewana na kutatua migogoro kwa kuzungumza na si kugombana. Amewaahidi wana Mafizi kuwa vijiji takribani 35 ambavyo havijapata usajiri atavifanyia kazi pamoja na timu ya watalaam wa Ardhi, Pia Mhe. Nickson alizungumzia vema Kauli mbiu ya Malisho Maji na Masoko akisema kwa ujumla zinaunda “MMM”, na kusema serikali itapambana kuhakiksha Malisho yanapatikana, Pia alisema hatua ya kupata Hati inasogeza hatua ya pili ya kupata Masoko. Mhe. Nickson alisema anapenda taarifa na amesema mwananchi yeyote anaweza kumpigia.

Aidha Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya maeneo ya wafugaji na kuona miradi mbalimbali na baadhi ya maeneo ya malisho ya wanyama.


Zoezi la Ugawaji wa Hati lilihitimishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Mhe. Zuberi Kizwezwe, ambaye aliwakumbusha wananchi kuambatana na kufanya kazi kwa bidii na kuepukana na migogoro pia alimpongeza Diwani wa Kata ya Mafizi Mhe. Yadhamen Jamal Nghonde kwa juhudi zake katika Kata ya Mafizi.

Mhe. Kizwezwe aliwashukuru wana Mafizi na kuhitimisha zoezi hilo.


Imeandaliwa na kitengo cha TEHAMA na Mahusiano

Announcements

  • Wito Kwenye Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari tarehe 10-11/02/2025 Minaki Sekondari. February 07, 2025
  • Tangazo kwa Umma Kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura February 08, 2025
  • MKITANO WA BARAZA LA MADIWANI April 28, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 2021 November 09, 2021
  • View All

Latest News

  • NIMEFURAHISHWA NA MMLIVYOJIPANGA KISARAWE CHATANDA NA ZAINABU

    May 08, 2025
  • OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS SERIKALI MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA KISARAWE

    April 30, 2025
  • KISARAWE YAFANYA UTOAJI ELIMU YA DOZI YA NYONGEZA YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO(IPV2)

    April 30, 2025
  • KUVUNJWA KWA BARAZA LA MADIWANI KISARAWE UONGOZI WAJIVUNIA KUKAMILISHA MIRADI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5

    April 29, 2025
  • View All

Video

Kamati ya Fedha kutembelea Ujenzi wa Jengo Jipya la OPD Kisarawe Hospitali
More Videos

Quick Links

  • Natural Attractions
  • COMMUNITY HEALTH FUND
  • Kisarawe History
  • Photo Events in the Council
  • Rehabilitation of Theater Block
  • Council strategics
  • How to meet with District Chairman
  • Maelekezo jinsi ya kutumia Mfumo wa FFARS
  • Councilors Name List and Phone Number

Related Links

  • President's Office Public Service, Management and Good Governance
  • The National Examinations Council Of Tanzania
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • The Higher Education Students’ Loans Board
  • PPRA
  • State House
  • Employment
  • National Bureau Of statistics
  • Salary slip potral
  • Government Website
  • Parliament
  • Mfumo wa Ununuzi wa Umma NeST
  • Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (ESS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.