Mheshimiwa Bi. Theresia Louis Mmbando ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani atembelea Wilaya ya Kisarawe. Ziara hii ni kati ya ziara zake za kawaida katika kuzitembelea Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani. Lengo kuu la kutembelea ni kujitambulisha na kusikiliza kero mbali mbali za watumishi wa kila Halmashauri. Akiongea na watumishi wa Kisarawe Bi. Theresia Louis Mmbando aliwahimiza watumishi kufanyakazi kwa juhudi.Katibu Katibu Tawala aliwakumbusha watumishi kuwa wamepata bahati ya kuwepo katika halmashauri hii wala zoezi la vyeti feki halijawakumba hivyo wajitume na wawe na moyo wa kupenda kazi waliyonayo. Pia Bi. Theresia Louis Mmbando aliwashauri watumishi wanaotaka kujiendeleza wajiendeleze katika maeneo ambayo yana upungufu akitolea mfano watumishi wakasomee masoma ya uhandisi.
Bi. Theresia Louis Mmbando alisikiliza kero mbali mbali zikiwemo (1) Upungufu wa vitendea kazi katika Idara ya Ujenzi (2) Kupandishwa madaraja kwa watumishi na Kuabadilishwa kwa Muundo. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ndugu Musa Gama alitoa majibu ya upungufu wa vitendea kazi alisema mpango upo kwa ajili ya manunuzi ya Gari jipya ambalo litatumika kwenye usimamizi wa Mapato na shughuli nyingine za Ujenzi.Pia kuhusu kupanda kwa madaraja ya watumishi Afisa Utumishi Ndugu Patrick Saduka kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji(W) alijibu kuwa mara ya mwisho madaraja ya watumishi yalipandishwa mwaka 2015.Ndugu Saduka alisema kwa sasa kupandishwa kwa madaraja yamesitishwa kwa sababu ya uhakiki unaoendelea. Pia Saduka alisema swala la recategorization kwa watumishi lipo kwenye mchakato wanasubilia kibali toka kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Mwisho Bi. Theresia Louis Mmbando aliwashukuru watumishi kwa kutoa muda wao wa kumsikiliza na kuwasisitiza wawe waadilifu katika Utumishi wa Umma.