Tarehe 8.10.2019 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Joketi Mwegelo atazindua barabara ya kutoka Kisarawe kwenda Nyerere National Park.Hivyo wananchi na wadau wa utalii mnakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria ndani ya Wilaya yetu. Tukio hili litaanzia pale Minaki sekondari saa mbili asubuhi kisha kutembelea Vivutio vya Utalii katika Msitu wa Pugu.Mara baada ya kutembelea vivutio vya utalii uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Mkuu wa Wilaya atapokea taarifa ya Utalii na risala toka kwa chama cha waongoza Watalii.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa