Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ina eneo lipatalo hekta 353 500, (3,535 Km2) ambapo eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 380,000 kati ya hizo kiasi cha hekta 30 000 ndilo linalolimwa, (NBS, 2002).
Wilaya ya Kisarawe inapata mvua za aina mbili ( i ) mvua za muda mfupi yaani mvua za vuli ambazo hunyesha muda mfupi kuanzia mwezi Octoba na kuishia mwezi Disemba na (ii ) mvua za muda mrefu yaani mvua za masika, mvua hizi huanza mwezi march na kuishia mwezi Juni. Wastani wa mvua zinazonyesha wilayani kwa mwaka ni mm 1,400 hadi mm 1,600 kwa upande wa mashariki wa wilaya ambayo ni maeneo ya tarafa ya Sungwi, na maeneo ya magharibi ambayo ni Chole na Mzenga yanapata mvua kidogo kiasi cha mm 1,000 kwa mwaka, (KDC, 2010).
Picha na. 1: Kituo cha upimaji wa hali ya hewa Kisarawe
2 Nyuzi joto
Nyuzijoto ni kiwango cha ubaridi au joto la kitu husika mfano mwili wa binadamu. Eneo lipo katika mwiinuko wa mita 150 hadi 900 kutoka usawa wa bahari. Hivyo eneo lina nyuzijoto kati ya 280C hadi 330C kwa wastani wa nyuzijoto 30.50C.
Kutokana na sensa ya taifa ya idadi ya watu mwaka 2012 wilaya ilikuwa na idadi ya watu wapatao 101 598 na kiwango cha ukuaji wa watu ni wastani wa asilimia mbili pointi moja kwa mwaka (2.1%). Inakadiriwa kuwa kiwango cha idadi ya watu kinaweza kufikia 108,472 ifikapo mwaka 2018. Idadi ya wanawake ilikuwa 50,967 Wanaume walikuwa 50,631 idadi ya kaya ilikuwa 26,051. Wastani wa ukubwa wa kaya moja ilikuwa ni 3.9, (KDC, 2017).
Picha na. 2: Ramani ikionyesha wilaya ya Kisarawe
KILIMO;
Wilaya ya Kisarawe ina eneo kubwa ambalo lina rutuba ya kutosha ya kuotesha mazao mbalimbali lakini eneo hili halijaweza kutumiwa vya kutosha na wakazi ili waweze kuzalisha chakula cha kutosha. Katika eneo lote linalofaa kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo asilimia saba nukta tisa ( 7.9%) ndilo ambalo huwa linatumika, (URT, 2007). Kwa wakazi wa wilaya ya Kisarawe asilimia tisini na tano (95%) ya wakazi hutegemea shughuli za kilimo kuendesha maisha. Wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo wakijihusisha na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Zao kuu la biashara wilayani ni korosho, Muhogo ukiwa kama zao kuu la chakula na upande mwingine bisahara. Mazao mengine yanayolimwa ni mahindi, mpunga, mtama, ndizi, viazi vitamu, nazi na mbogamboga. Pia wilaya inafursa ya mazao mengine yakiwemo matunda kama vile Embe, Machungwa, Fenesi, Passion, Nanasi na “Citrus”, (KDC, 2017). Soko kubwa la mazao yanayozalishwa wilaya ya Kisarawe ni Dar es salaam and Kibaha.
MNYORORO WA THAMANI WA ZAO LA MUHOGO
Mhogo ndio zao kuu la chakula na pia zao la biashara na ni zao lililochaguliwa na Halmashauri kama ni zao la mnyororo wa thamani la Wilaya. Zao hili linakabiliwa na tatizo la kushambuliwa na magonjwa ya batobato (CMD) na michirizi ya kikahawia(CBSD); kwa hali hiyo Halmashauri imehakikisha uwepo wa ubora wa zao la muhogo kupitia uliokuwa Mradi wa kushirikisha Jamii kutambua na kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mhogo (Cassava Community Phytosanitation Project).
Kisarawe ni moja kati ya wilaya 4 ambazo zimetekeleza mradi huo. Wilaya nyingine ni Chato, Muleba na Mkuranga. Katika kutekeleza hilo kumeanzishwa mashamba darasa matatu katika Kijiji cha Mhaga kwa kupandwa mbegu bora ya mhogo yaani Kibaha 026 (KBH O26) na Kiroba kutoka kituo cha utafiti Kibaha (SRI) zenye ukinzani na maambukizi ya magonjwa ya batobato na michirizi ya kikahawia. Katika mradi huo wakulima walipata fursa ya mafunzo mbalimbali kuhusiana na kilimo cha mhogo kwa kutumia mbegu zisizo na maambukizi ya magonjwa ya batobato na michirizi ya kikahawia na namna ya kupunguza maambukizi. Pamoja na mashamba darasa 3 ya ekari moja kila moja kwa kila kitongoji na shamba la mbegu ekari 5 bado mahitaji ya mbegu ya mhogo kwa wakulima ni makubwa maeneo mengi ya wilaya yameathirika na magonjw hayo. Kwa sasa wilaya ina mpango wa kuhamasisha jamii ili kila Kata kuwepo na Kijiji kimoja kitakachokuwa na Kikundi kitakachopata mafunzo kuhusiana na zao la mhogo na kusimamia shamba la mbegu na hatimaye kuweza kuwa na mbegu isiyo na maambukizi ya kutosheleza na kusambaza mbegu hiyo kwenye vijiji vingine vya Kata husika kwa gharama nafuu.
Picha na. 3.: Wataalam wakilimo na baadhi ya wakulima wakiwa wametembelea shamba darasa la Mhogo
Picha na. 4: Shamba darasa la mhogo kijiji cha Mhaga lililopandwa mbegu aina ya Kibaha 026
Picha na. 5: Shamba la mbegu ya Mhogo lililopandwa mbegu aina ya Kibaha026
Vilevile mradi umeweza kuwaelimisha wakulima namna ya usindika zao la mhogo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuweza kujiongezea kipato.
Picha na. 6: Wakulima kijiji cha Mhaga wakiwa kwenye mafunzo ya usindikaji
Picha na. 7: Siku ya wakulima Kijiji cha Mhaga. Wanakukundi wakionyesha bidhaa zitokanazo na Mhogo
ZANA ZA KILIMO
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans – DADPs) imeweza kuviwezesha Vijiji kwa kuvipatia zana za kilimo aina mbalimbali. Maudhui makuu ya kuwepo kwa zana hizi ni kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la muhogo.
Zana za kilimo zilizosambazwa vijijini ni pamoja na matreka makubwa manane (8), Vituo vya usindikaji wa zao la muhogo tisa (9), mashine za kuchakata muhogo kumi na mbili (12), mashine za usindikaji wa mazao ya mafuta tatu (03), na matrekta ya mkono (powertiller) ishirini na nne (24).
MATREKTA MAKUBWA.
Matrekta makubwa manane yaliyopo yalikabidhiwa Vikundi ambavyo viliteuliwa na Kijiji kupitia Mikutano Mikuu ya Vijiji husika. Kati ya matrekta hayo manane, manne yalinunuliwa na kumilikiwa na Vikundi vya Usindikaji wa muhogo vya Kisanga, Zegero, Mhaga, na Kidugalo Chakanga. Matrekta mengine manne yalikabidhiwa Vikundi vya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika Vijiji vya Kwala, Kazimzumbwi, Msimbu na Marui Mgwata.
VITUO VYA KUSINDIKA ZAO LA MUHOGO
Vituo tisa vya kusindika zao la muhogo vinakamilishwa kuwepo kwa vifaa maalum vikiwemo jengo, trekta, mashine ya kuchakata muhogo “Crater”, mashine ya kutengeneza chips “Cheaper”, Mashine ya kusaga muhogo “Milling machine” na mashine ya kukamulia muhogo uliochakatwa “Pressor mashine”.
MASHINE ZA KUCHAKATA NA KUKAMULIA MUHOGO
Mradi huu ulinunuliwa vifaa vya mashine ya kuchakata muhogo “Crater”, na mashine ya kukamulia muhogo uliochakatwa “Pressor mashine”.
Vijiji kumi na mbili (12) vilivyowezeshwa kununuliwa mashine za kuchakata muhogo ni vijiji vya Gumba, Kibuta, Mtamba, Maguruwe, Chang’ombe B, Bembeza, Titu, Kihare, Chole, Kazimzumbwi, Mhaga, na Marumbo.
MASHINE ZA USINDIKAJI WA MAZAO YA MAFUTA
Vijiji vitatu vya Vikumburu, Mfuru na Kikwete vina mashine za usindikaji wa mafuta kama ifuatavyo:-
MATREKTA YA MKONO (POWERTILLERS).
Matrekta ya mkono (powertiller) ishirini na nne (24) yakiwemo matatu yaliyopo kwenye vituo vya kilimo vya Kibuta, Mafumbi na Mzenga. Vijiji vilivyonufaika na zana hizi ni Mzenga, Mafizi, Nyani (2), Mianzi, Vihingo, Kurui, Marumbo, Msanga, Maneromango, Chole, Marui, Vikumburu, Msimbu, Kisarawe, Kibuta Masaki, Kiluvya, Mitengwe.
Picha na. 8: Kikundi cha Mshikamano (Wanawake ) cha uchakataji muhogo cha wa kijiji cha Kitanga
Picha na.9.: Trekta la Kikundi cha Mshikamano (Wanawake ) cha uchakataji muhogo cha wa kijiji cha Kitanga
VITUO VYA KILIMO (Ward Agricultural Resource Centre - WARCs)
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Programme - ASDP) ilibuni mradi wa Kujenga Vituo vitatu vya Rasilimali ya Kilimo vya Kata (Ward Agricultural Resource Centre - WARCs) katika Kata za Mzenga, Kibuta na Chole (Mafumbi).
Utekelezaji wa Mradi huu ambao ulifanyika kwa awamu, ulianza katika mwaka wa fedha 2010/11 ambapo kiasi cha Shilingi 72,000,000/= zilipokelewa kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vituo. Awamu ya pili katika mwaka wa fedha wa 2014/15 Halmashauri ilipokea shilingi 330,000,000/= ambazo zilitumika kumalizia ujenzi wa vituo, maandalizi ya mashamba darasa, kununulia samani, Kompyuta, jenereta na Trekta 3 za mikono aina za power tiller.
Kwa mujibu wa Mwongozo wa kuanzisha na kuendesha Vituo vya Rasilimali za Kilimo vya Kata (Ward Agricultural Resource Centre – WARCs) wa mwaka 2008 Ukamilifu wa Vituo hivi ni kuwepo kwa eneo la kutosha kati ya hekta 1-2 litakalowezesha kukamilishwa kwa mambo yafuatayo:-
Kuwepo kwa Jengo la Ofisi lenye Chumba cha nafasi ya kutosheleza wataalam angalau sita wa Kilimo, Mifugo na Ushirika, ukubwa wa kutosheleza kuweka kompyuta angalau sita; Chumba cha maktaba kwa ajili ya kutunza vitabu, majarida na taarifa mbalimbali na kiwe na ukubwa wa nafasi inayoruhusu angalau watu 15 kujisomea kwa wakati mmoja; Chumba cha mikutano na mafunzo chenye uwezo wa kuchukua angalau watu 40 kwa wakati mmoja; Maabara ndogo itakayowezesha kufanya uchunguzi wa awali wa sampuli za mimea, mifugo na kutunza dawa za chanjo na kutoa huduma ya Uhimilishaji (Artificial Insemination); na Stoo inayotosheleza kuhifadhi vifaa na pembejeo.
Kuandaa mashamba ya maonesho kwa ajili ya mafunzo na yanayoendeshwa kibiashara.
Maliwato: bafu na choo chenye matundu manne yanayozingatia jinsi
Banda/karakana ya kuhifadhia zana za kilimo na mifugo;
Kibanio cha mifugo (cattle crush).
Mabweni mawili (me na ke) ya kutosha watu 20 kila moja kwa ajili ya malazi ya wakulima wakati wa mafunzo yatakayolazimu kulala kituoni;
Jukumu la Halmashauri ya Wilaya ni kuwezesha katika ujenzi, vifaa, habari na teknolojia.
Mambo ya msingi yaliyokwisha fanyika ni upatiknaji wa eneo la kutosha katika kila kituo, ujenzi wa Ofisi zenye kukidhi haja, maeneo ya shamba darasa, ununuzi wa vifaa/zana za kilimo (matrekta ya mkono), samani na maliwato zimejengwa. Mahitaji mengine (iv – vi) bado kukamilishwa. Aidha bado kukamilishwa Maabara ndogo na Stoo.
Kutokana na mapungufu hayo makubwa Vituo hivi bado kukamilika.
WARCs za Mafumbi, Kibuta na Mzenga katika mwaka wa 2014/15 zilianza kutoa mafunzo katika kipindi cha masika kama ifuatavyo:-.
Mafunzo hayo yalitolewa bila ya kuwepo kwa bajeti ya Halmashauri ikiwa ni juhudi binafsi za Ma afisa Ugani wa maeneo husika.
Aidha Vituo vya kilimo hufanya kazi nyingine zikiwemo za walengwa kutembelea vituo na kupata mafunzo kupitia maandiko ya kilimo bora cha mazao mbalimbali ambapo pia huweza kuazimwa vitabu hivyo. Pia kumbi zilizopo zinatumika kuendeshea mafunzo pale ambapo yanapopata mgharamiaji. Shughuli nyingine za ugani zilizoendeshwa kwa mwaka 2015/16 (kiangazi) ni kama zifuatazo:-
Changamoto:-
Pamoja na Vituo kuanza kutoa mafunzo vilikuwa na changamoto zifuatazo:-
Matarajio 2016/17
Kwa mwaka huu 2016/17 Halmashauri imeweka bajeti ya sh. 2,384,788/= Kwa kila Kituo kwa ajili ya mbegu na pembejeo. Fedha hizi zinatarajiwa kutokana na bajeti ya miradi ya maendeleo zitakazopatikana kutoka mapato ya ndani (own source).
Picha Na 10: Kituo cha kilimo cha kata ya Kibuta.
Picha Na 11: Mafunzo ya uanzishaji vitalu vya miche bora ya korosho Kibuta.
Takwimu za uzalishaji mazao;
Aina ya zao
|
2007/08
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
2013/14
|
Muhogo
|
66,857 |
63,036.4 |
240.9 |
10,045 |
25,772.4 |
8,340 |
36,450 |
Mahindi
|
814.5 |
7,506 |
1,208.2 |
1,444.6 |
1,278.2 |
4,306 |
3,454 |
Mtama
|
2,290 |
1,610 |
35.8 |
48 |
900 |
610 |
261 |
Mpunga
|
8,500 |
722 |
891.3 |
110 |
365 |
1,069 |
590.4 |
Mikunde
|
4,603 |
3,493.5 |
197.8 |
568.6 |
975.8 |
1,120 |
178.1 |
Viazi vitamu
|
6,000 |
34,200 |
3,170.7 |
355.5 |
3,650 |
1,326 |
1,380 |
Jumla
|
89,064.5 |
110,567.9 |
5,744.7 |
12,571.7 |
32,941.4 |
16,771 |
42,313.5 |
Jedwali na 1. Takwimu ya uzalishaji ( kwa tani) 2007 – 2014.
Picha Na 12: Maafisa kilimo walipomtembelea mkulima wa mpunga kijiji cha Kihare
Picha Na 13: Shamba darasa la zao la nyanya eneo la Kisarawe Nanenane mjini Morogoro.
TAKWIMU YA UZALISHAJI WA MATUNDA 2007 – 2014
Aina ya zao
|
2007/08
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
2013/14
|
Machungwa
|
657 |
692 |
1,140 |
1,148 |
1,158 |
1,158 |
1,158 |
Embe
|
1,163 |
1,165 |
1,166 |
1,173 |
1,173 |
1,182 |
1,190 |
Nazi
|
7,680 |
7,810 |
7,992 |
7,998 |
8,753 |
8,753 |
8,760 |
Chikichi
|
1,251 |
1,370 |
1,270 |
1,370 |
1,370 |
1,370 |
1,370 |
Korosho
|
975.64 |
1,050 |
1,150 |
1,300 |
28 |
810 |
670 |
Jumla
|
11,726.64 |
12,370 |
12,718 |
12,989 |
12,482 |
13,273 |
13,148 |
Jedwali na. 2: Takwimu ya uzalishaji wa matunda Kisarawe
Picha Na 14: Shamba la miembe kata ya Kurui
UMWAGILIAJI;
Wilaya ya Kisarawe ina maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji yapatayo hekta 5,000 kati ya hizo hekta 40 ndizo ambazo zipo chini ya maandalizi kwa ajilia ya umwagiliaji eneo hilo lipo kijiji cha Mianzi kata ya Msanga.
Wilaya imepanga kutumia eneo la umwagiliaji kwa kuchukua maji kutoka katika mto kwa kutumia miundombinu yenye thamani ipatayo 3,600,000,000 pesa za kitanzania. Utekelezaji wa mpango huu unatarajiwa kuanza pindi pesa itakapopatikana.
Maeneo ambayo umwagiliaji unaweza kufanyika kisarawe.
s/n |
Scheme |
Start of farmland
|
Intake site |
||
Latitude |
longitude |
Latitude |
longitude |
||
1. |
Mafizi
|
E.038.56096o
|
S.06.99986o
|
E.038.55953o
|
S.07.000660
|
2. |
Marui – Mipera (Mtuna bwawani)
|
E.038.767260
|
S.07. 354870
|
E.038.767350
|
S.07.354110
|
3. |
Marui – Mipera (Mkongoroni)
|
E.038.765170
|
S.07.343820
|
E.038.7653380
|
S.07.343910
|
4. |
Marui – Ngwata (kisoti bwawani)
|
E.038785180
|
S.07.380670
|
E.038.785770
|
S.07.380690
|
5. |
Mianzi
|
E.038.781730
|
S.07.305290
|
E.038.781530
|
S.07.304500
|
6. |
Nyani
|
E.038.538400
|
S.07.051730
|
E.038.531890
|
S.07.049270
|
Jedwali na. 3: Takwimu za Maeneo ambayo umwagiliaji unaweza kufanyika kisarawe
Maeneo mengine sita yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambayo hayajafanyiwa uhakiki ni Gwata, Ving’andi, Bwama Doloto, Kimalamisale na Mihugwe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa