Mkuu wa idara Ndugu Generosa Nyoni
Idara ya elimu sekondari ni miongoni mwa idara kumi na tatu zilizopo katika halmashauri. Idara hii inazo shule za sekondari 21 zikiwemo za serikali 15 na za Binafsi 6. Kati ya shule hizo za serikali moja ni ya bweni na ni ya kidato cha tano na sita pekee.
Wilaya ina jumla ya wanafunzi 4,604 shule za serikali wakiwemo wavulana 2,646 na wasichana 1,958. Na wanafunzi 1,033 shule za Binafsi wakiwemo wavulana 728 na wasichana 310 . Aidha wilaya inao walimu 522 katika shule za serikali wakiwemo wa shahada 345 na stashahada 185. Kati ya walimu hawa tunao upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati wapatao 100.
Katika kutekeleza shughuli zake idara inawajibika katika
Aidha shughuli nyingine ni kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu mbalimbali zihusuzo shule kwa ujumla wake pamoja na kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari katika Wilaya.
Katika kutekeleza shughuli hizo Halmashauri imendelea kupandisha kiwango chake cha ufaulu k.m Kidato cha pili kimeendelea kupanda mwaka hadi mwaka 2012 asilimia 48.4, 2013 asilimia 62.7 na mwaka 2014 asilimia 87 na mwaka 2015 asilimia 82. Kidato cha nne matokeo yamekuwa asilimia 31.3 mwaka 2012, asilimia 46.3 mwaka 2013, asilimia 71 mwaka 2014 na mwaka 2015 asilimia 58. Hata hivyo kwa Kidato cha sita maendeleo yamekuwa asilimia 93 mwaka 2013 , 2014 asilimia 95 na mwaka 2015 asilimia 98.
Halmashauri imeendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule kama vile madarasa, yamejengwa 171 kati ya 226 ambayo yanatosheleza kwa idadi ya wanafunzi waliopo, maabara zipo 32 kati ya 45, vyoo matundu 226 kati ya 385 na nyumba za walimu 78 kati ya 522 ili kuzifanya shule kuwa shule zenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia.
Maabara katika moja ya shule za Sekondari
Halmashauri imeendelea kupokea fedha za elimu bila malipo ambazo hupitia katika akaunti za shule kila mwezi na kuziwezesha shule katika masuala ya kiuendeshaji, ununuzi wa vifaa na kemikali pamoja na chakula cha wanafunzi wa bweni. Kuanzia januari hadi aprili tumepokea kiasi cha shilingi 168,379,000.00 zikiwemo shs. 106,394,000.00 za chakula, shs. 30,881,000.00 za capitation na fidia ya ada shs. 31,104,000.00
Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Baadhi ya changamoto hizo zinazokwamisha mafanikio ni
• Uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu na vifaa vya maabara
• Ukosefu wa miundombinu ya kutosha na iliyo bora kama vyoo, ofisi, nyumba za walimu, maktaba na maabara. Tatizo hili linafanya
o walimu wengi kukaa mbali na shule hivyo kushindwa kuwasaidia vijana wetu kwa ufanisi kutokana na kukosa muda
o Walimu kukosa mahali pazuri pa kujiandalia na hivyo kushindwa kutoa kinachotakiwa kikamilifu.
o Tatizo la vyoo husababisha baadhi ya wanafunzi kuwa watoro
• Wanafunzi kuishi mbali na shule na hata shule zilizo na hosteli wanafunzi kutozitumia hii hufanya muda mwingi watembee na wasikazanie masomo.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa