Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe kupitia kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO inapenda kuwaelekeza watumishi ambao wanahitaji kupata nakara ya mshahara/ salary slip kuwa inapatikana kupitia mfumo.
Ili kupata nakara ya Mshahara unatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa Watumishi Portal. Kwenye mfumo huu wa watumishi utakuwezesha kupata taarifa zako za kiutumishi.
Vitu vya kuzingatia:
Ili kujisajili Bofya hapa.Kujisajili kwenye mfumo
Pia unaweza kupata stakabadhi yako ya mshahara kwa kutumia mfumo mpya wa "Government Salary Slip Portal" ambapo utajisajili kwenye mfumo.
Kwenye Mfumo huu vitu vya kuzingatia ni:
Kama wewe ni mtumiaji wa mara ya kwanza lazima kwanza ujisajili. Ili kujisajili Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Manage/EmployeeRegistration
au kuingia kwa waliojisajili kwenye Government Salary Slip Portal Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Account/Login?ReturnUrl=%2F
Kumbuka siku zote check namba yako ndio username yako. Hakikisha unauhakika na cheki namba yako.
PIA UNAWEZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO MPYA WA ESS ILI UWEZE KUOMBA UHAMISHO NA KUPATA SALARY SLIP.
BONYEZA HAPA------>https://ess.utumishi.go.tz/
Unaweza Kufika kwenye ofisi zetu za TEHAMA na UHUSIANO Kisarawe kwa msaada zaidi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa