Mapinduzi ya matumizi ya TEHAMA hasa mitandao ya kijamii kwa vijana yanalenga kuzalisha vijana wabunifu wa masuala ya TEHAMA ambao watatengeneza mifumo ya kimtandao ama maunzi laini (Applications) zitakazowezesha jamii kupata na kutumia katika huduma mbalimbali, mfano mfumo wa mtandao wa Maxmalipo umewezesha jamii kufanya malipo ya huduma za kijamii ikiwemo maji na umeme bila mteja kwenda kwenye kituo cha huduma husika hivyo kuokoa muda na kutatua dharura.
Halikadhalika, serikali inaweza kutumia fursa hiyo ya mitandao ya kijamii kwa kuchochea maendeleo kwa wananchi, kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa vijana kuwa wabunifu na kufanya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Mitandao ya kijamii ilianza kutumika nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo inatumika kwa kiasi kikubwa katika kuwasiliana, kubadilishana ujuzi na kutumika katika miamala mbalimbali ya fedha. Mitandao hii imebadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya watu katika nyanja mbalimbali mfano kitaaluma, biashara na mawasiliano.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa