ARO KATA JIMBO LA KISARAWE WALA VIAPO
Leo tarehe 04 Agosti, 2025
Hakimu Mkazi Mwandamizi wilaya Kisarawe Mhe. Emmy A.Nsangalufu amewaapisha Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata 34 (ARO KATA) wa Kata 17 zilizopo jimbo la Kisarawe katika Wilaya ya Kisarawe,
Mhe. Nsangalufu amewasisitiza Wasimamizi Hawa ngazi ya Kata kusimamia Sheria na taratibu kwani zoezi hili la kupiga kura ni Msingi wa Haki ya Kila mmoja.
![]() |
Aidha Msimamizi Jimbo la Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya Ndugu Sabra C Mwankenja amewasihi Maafisa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata zote 34 kuzingatia Viapo walivyo apa pamoja na maelekezo yanayotolewa,
![]() |
![]() |
"Nina uhakika mtakwenda kutimiza wajibu Kwa kufuata Yale yote mazuri ambayo mmevuna hapa kwenye mafunzo mliopata katika kufanikisha zoezi la kupiga Kura." Amesema Mwankenja
Semina hii inafanyika Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Kisarawe.
Zoezi hili litafanyika kwa mujibu wa sheria, na kuratubiwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na kaulimbiu ya zoezi hili ni
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa