ASANTE SANA DIRECT AID KWA ZAHANATI YA YA KISASA-DKT JAFO
NA
Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (Mb) Mhe DKT SELEMANI SAIDI JAFO amewashukuru Taasisi ya DIRECT AID kwa kuwajengea wanakisarawe Zahanati ya kisasa ambayo inatarajiwa Kumaliza shida iliyokuapo kabla Boga,
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Zahanati hiyo ya kisasa alifafanua kuwa inapaswa kutunzwa mazingira yake na kuhudumia wananchi Kama lengo lililokusudiwa kwa matokeo mazuri,
"Ndugu zangu wa kata ya Boga Zahanati hii ya kisasa kabisa Kisarawe kujengwa kwa ramani basi ikaendane na ubora wa huduma mbalimbali zitolewe kwa wananchi wa hapa kwa matokeo mazuri" alisisitiza Mhe Dkt Jafo,
Nae kwa upande wake akizungumza Wakati wa shughuli hiyo Meneja wa DIRECT AID Tanzania Ndugu Mohammed alisisitiza kuwa wao wapo tayari kujenga Nyumba ya mtumishi Kama walivyoombwa na Mhe Dkt Jafo,
"Sisi tumepokea kwa Wakati ombi lako Mhe Dkt Jafo la kujenga Nyumba ya Mtumishi hapa hivyo tunaenda kulifanyia kazi na Insha Allah tutatekeleza kwa Wakati kuwasaidia wananchi hapa Boga" alimalizia Ndg Mohammed,
Hata alisisitiza kuwa Zahanati hiyo ya kisasa imegarimu Jumla la shilingi Millioni Mia Moja na Sabini mpaka kukamilika kwake huku Vifaa tiba mbalimbali vikiwa tayari kwa kutumika.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa