Leo tarehe 1/12/2021 Balozi wa Uturuki nchini Tanzania amefanya ziara fupi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.Katika ziara hiyo Mhe. Balozi wa Uturuki amekabidhi jiko la kisasa la kuoka Mikate kwa kikundi cha KIWAWANYU,Jiko la gesi la kupikia Chapati kwa kikundi cha Vijana kilichopo kiluvya,kutembelea shule ya Msingi Kazimzumbwi na soko kuu la Kisarawe.Mara baada ya ziara Mhe Balozi aliahidi kuendelea kutoa misaada mingine kwa Wilaya ya Kisarawe.
Misaada iliyotolewa ipo chini ya shirika la TIKA.
Mbali na misaada hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Chini ya Mkurugenzi Mtendaji Hanan Bafagih imetoa msaada wa milioni 24 kwa kikundi cha KIWAWANYU ili iwasaidie katika kuendesha shughuli zao za uzalishaji.
Ziara hiyo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali na Kidini.
Imeandaliwa na kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO(W)-KISARAWE
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa