Katika kuhakikisha suala ya lishe bora kwenye michezo shuleni linakua lenye tija na Matokeo mazuri Bank ya DCB imeichangia idara ya elimu msingi na sekondari Jumla ya kg 100 za Mchele kwa ajili ya Watoto waliopo kambi ya Michezo iliyopo Shule ya Secondari ya Minaki kwa ajili ya Michezo ya Umisseta na Umitashumta kisarawe.
Akitoa Msaada huo kwa kisarawe kwa Niaba ya Meneja wa Bank Tawi la Chanika Bi Hellen Boyo alisema wameguswa na hali ya vijana wa kisarawe ambao wanashiriki katika michezo wilaya na kukakbiliwa na changamoto ya chakula
‘’Sisi kama Bank ya DCB ni wadau wakubwa wa maendeleo kwa wanafunzi hivyo kama bank ni wajibu wetu kuwaunga Mkono Idara ya Elimu Msingi na Sekondari Kisarawe katika michezo hasa hii ya umitashumta na umisseta ’’alisema Boyo
Nae Afisa Elimu Msingi wilaya Shomari Bane akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi aliwapongeza DCB kwa msaada wao huo na alitaka wadau wengine wa maendeleo kuchangia michezo hasa kwa vijana ambao wanavipaji vya michezo
’’Hapa Kisarawe kuna Vijana wana vipaji vizuri tu vya Michezo ila bado hawajapata Sapoti ili kuonyesha vipaji vyao nawashukuru DCB kwa kuonyesha njia ya kutoa Misada na Taasisi nyengine waige wenzao kama Bank DCB ’’ alisema Bane
‘’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa