Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kisarawe katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo ameipatia jumla ya shilingi milioni arobaini na nne laki nne, shule ya sekondari makurunge kwa ajili ya kujenga vyumba viwili vya madarasa mapya ya shule hiyo inayokabiliwa na uhaba wa madarasa ya kusomea wanafunzi iliyopo katika kata ya kiluvya tarafa ya sungwi
Akizungumza katika kikao cha elimu elekezi na uhamasishaji ujenzi wa mradi huo juu ya hatua za kufuata katika sharia ya manunuzi na ujenzi wa madarasa hayo ya vyumba viwili hapo makurunge afisa elimu sekondari wilaya mwalimu PATRIK GWIVAHA
“Alisema kwamba kwa ujumla huduma ya sekta ya elimu na afya inakua kila siku hivyo nayo mahitaji yake yanakua maana miundo mbinu iliyopo ni kidogo ukilinganisha na mahitaji ya sasa hivyo maboresho ni lazima yalingane na mahitaji na ndio maana Mkurugenzi wilaya akaamua kuipatia fedha shule hii ili kukabiliana na changamoto zlizopo makurunge”
“Ndugu zangu tupo hapa kuwakilisha kile ambacho mkurugenzi amekileta kwa wana makurunge ili kukabiliana na changamoto ya elimu na kuinua sekta ya elimu kwa kusimamia maendeleo ya elimu kwa vijana wetu”
Aidha Gwivaha aliitaka bodi ya shule hiyo ya makurunge na kamati ya ujenzi kusimamia sharia na kanuni za ujenzi na manunuzi kwa mujibu wa sharia za serikali kama inavyoelekeza katika ujenzi wa miradi ya serikali ili kuepusha usumbufu na lawama kwa mamlaka za usimamizi za serikali,sambamba na kufikia lengo kuu la ujenzi wa mradi huu wa kisasa.
‘’Ndugu wajumbe wa kamati na bodi ya shule nakuombeni sana Muhimu Mushirikiane katika ujenzi huu ili kufanikisha mradi huu kwa shule yetu kwa kuwashirikisha watalamu wa wilaya hasa kwa idara ya manunuzi na ujenzi kwa kila hatua ya mradi ,’’alisisitiza Guivaha
‘’ofisi ya Mkurugenzi ina watalamu hivyo naomba makurunge mushirikiane ili kuondosha urasimu wa katika ujenzi katika mradi huu ili uwe wa kitalamu kwa kuondosha minongono ya lawama baina ya watalaamu na wajumbe wa ujenzi wa mradi huu’’
Naye Kaimu afisa manunuzi wa wilaya ndg Mussa Maganga aliwambia wajumbe wa bodi na kamati ya ujenzi kuwa ofisi yake ipo tayari kutoa mashirikiano kwa manunuzi ya vifaa vya ujenzi kila hatua ya mradi ili kufikia lengo la mradi ambao unatarajiwa kuchukua muda wa miezi miwili kutoka sasa,
‘’Ndugu wa wajumbe muhimu tuzingatie sheria na kanuni za manunuzi na katika hili ofisi yangu itakua bega kwa bega na kamati teule katika kuhakikisha tunakamalisha mradi kwa wakati hapa makurunge ’’ alimalizia Maganga
Naye kaimu Mhandisi wa majengo kisarawe Eng Ernest Maungo alisisitiza ushirikiano katika kufikia ujenzi bora wa Viwango vinavyohitajika kwa mujibu wa sheria za majengo ili kuleta matokeo chanya ya majengo na miradi ya serikali inayopata fedha za mashirika au serikali pamoja na kuwashirikisha wananchi ili waweze kujua miradi iliyopo katika jamii yao,
Jumla ya shilingi bilioni moja zitatumika kujenga miundo mbinu ya elimu kwa shule za msingi na sekondari na sambabmba na vyoo na nyumba za walimu pamoja na vituo vya afya katika kata za msimbu,kibuta ,msanga,,mzenga ,masaki na vihingo kisarawe ambazo fedha hizo zintokana na mfuko wa PAY FOR RESULT (P4R),
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa