Katika kuhakikisha Kisarawe inatokomeza zero Halmashauri ya wilaya kupitia idara ya Elimu Sekondari imeanda Bonanza kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Mgeni rasmi Ndugu Mussa Gama ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alisema wanafunzi wawe na moyo wa kuthubutu na kutokata tamaa, aliyasema haya alipokuwa akihutubia katika bonanza lilofanyika kata ya kisarawe shule ya sekondari Minaki. Bonanza hili limedhaminiwa na wadau mbali mbali wa maendeleo ndani ya Wilaya ya Kisarawe wakiwemo NMB,CoCa Cola na metropolitan.
Bonyeza hapa kwa matukio ya Picha
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa